Mmiliki
wa Shule ya Msingi na Awali (International) ya Mount Zion iliyopo
Bahari Beach, Dar, Annah Mizighi Mwambili enzi wa uhai wake.
INASIKITISHA!
Mmiliki wa Shule ya Msingi na Awali (International) ya Mount Zion
iliyopo Bahari Beach, Dar, Annah Mizighi Mwambili, 47, (pichani) ameuawa
na mwili wake kutupwa ndani ya shule yake baada ya kupotea kwa zaidi ya
miezi sita huku mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Tatu Ntimizi, Said Ntimizi akidaiwa kuwa mmoja kati ya
watuhumiwa wa mauaji hayo.
Duru za awali za upelelezi wa polisi, zinamtaja Said kuwa alikuwa na
uhusiano wa karibu na marehemu bila kufafanua alihusikaje na mauaji hayo
ya kinyama yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana, siku na tarehe
isiyojulikana na mwili wake kutupwa kwenye shimo la maji taka ndani ya
eneo la shule aliyokuwa akiimiliki.Aidha, nyuma ya taarifa hiyo ya mauaji, deni la shilingi milioni mia tisa (900,000,000) ambalo mwanamke huyo alikuwa akimdai mmoja kati ya watuhumiwa hao ambao majina yao yote bado hayajafahamika likitajwa kuwa ndiyo chanzo cha Annah kutolewa uhai.