Waziri
wa Maendele Jamii Jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba (katikati)
akizungumza na waombolezaji waliofika nyumbani wa Marehemu,Eugen
Mwaiposa leo Mchana.
HII ndiyo tawsila ya Nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga jijini Dar baadhi ya watu pamoja na wabunge wakiendelea kujitokeza kwa ajili ya kuifariji familia ya Mume wa marehemu,Ally Mwaiposa.
Akizungumza na wanahabari mmoja wa wanandugu wa familia hiyo, Fitina Mkandala alisema kuwa mwili wa Marehemu unatarajiwa kuzikwa Juni 6 mwaka huu, lakini akasema kuwa ,ratiba kamili ya mda wa mazishi itatolewa kufuatana na utaratibu wa sheria za Bunge, huku akisema kuwa watoto wa marehemu nao wanatarajia kufika kesho wakitokea masomoni, nchini Canada na mwingine akitokea Uingereza.
Mwili wa Marehemu Eugen unatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Kipunguni ‘A’Matembele-Ukonga jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment