Kama uko karibu sana na TV za Kimataifa kama BBC, Sky News na CNN
utagundua kwamba kwenye stori kubwa zilizopewa headlines sana iko ya
Shambulio la Kugaidi lililotokea Tunisia na kusababisha mauaji ya
Watalii.. Breaking News imeingia
nayo kwenye stori kubwa zilizo kwenye headlines sasahivi, inahusu Ndege
ya Kijeshi kuanguka kwenye makazi ya watu Indonesia na watu
30 wamefariki.
Ndege hiyo ilipata ajali muda mfupi baada ya kuruka kutoka kwenye Uwanja wa Medan Polonia Airport.
.
ndani ilikuwa imebeba jumla ya watu 12, ndege imeanguka kwenye mtaa
ambao una makazi ya watu pamoja na Hoteli, gari moja pia limewaka moto
baada ya kutokea ajali hiyo.. eneo lote la ajali limeshika moto.Wenyeji wa eneo hilo wamesema hii ni mara ya pili kwa nyumba za eneo hilo kuangikuwa na ndege, iliwahi kuanguka Boeing 737 mwaka 2005 ikaua watu 143 na kati yao watu 30 walikuwa ni watu ambao wanaishi eneo hilo, hawakuwemo ndani ya ndege.
Vikosi vya Zimamoto na Uokoaji vinaendelea na kazi ya kuzima moto pamoja na kutoa miili ya watu waliofariki kwenye ajali hiyo, huenda idadi ya waliofariki na majeruhi ikaongezeka wakati wowote kuanzia sasa.
0 comments:
Post a Comment