Friday, June 26


Siku chache zimepita tangu hukumu ya kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kutolewa dhidi ya mzazi mwenzake Faiza Ally,baada ya kuiomba mahakama kumchukua mtoto wao, hali iiyopelekea mahakama kutoa hukumu kuwa mtoto achukuliwe na Mbunge huyo,  jambo lililofanya sakata hilo kutinga bungeni.
 
Baadhi ya wabunge na wadau mbalimbali wamedai kuwa mtoto bado ni mdogo sana kuweza kuishi na baba yake na kutoa maoni kuwa mtoto arudishwe kwa mama yake kwa kuwa kila mtu ana mapungufu na kusema kuwa mtoto bado ana haki ya kuwa karibu na mama yake.
 
Kwa mujibu wa Mbunge Martha Mlata jana  alisema kuwa; “Tuna Mbunge mwenzetu amemnyanyasa mwanamke mwenzetu ametumia siku moja Mahakamani kumnyang’anya mtoto wa miaka miwili.. Mbunge huyu anajijua kwa sababu mwanamke huyo anaitwa Faiza.. Faiza arudishiwe mtoto wake”.
 
Hoja hiyo ikachangiwa na Mbunge David Kafulila alisema “Hii nchi ina mihimili mitatu, Bunge, Mahakama na Serikali… Tuheshimu maamuzi ya Mahakama”.
 
Sambamba na hilo Waziri Saada Mkuya akahitimisha na kusema; “Kama mama na mimi nilipoisikia ile taarifa nilipata uchungu, kila binadamu ana mapungufu yake lakini mtoto alelewe na mama yake”.

0 comments:

-