Monday, June 29

aunt na iyobo-002 
Mkali wa sinema za Kibongo Aunt Ezekiel akiwa na wafanyakazi wa Globalpublishers walipomtembelea kumuona mtoto wake.
Makubwa! Aunt Ezekiel ameweka wazi kinachotafsirika kuwa ni kuzaa nje ya ndoa huku akishikilia alichokiita ‘hayo ni mambo yake binafsi’, Ijumaa Wikienda liligaragazana naye kwa maswali. 
Akizungumza kwa njia ya simu na ‘kijumbe’ wetu wikiendi iliyopita, mkali huyo wa sinema za Kibongo, alisema kamwe hapendi kuulizwa masuala ya ndoa yake.
aunt na iyobo 
Aunt Ezekiel na mume wake Moses Iyobo wakifurahia na mtoto wao.
Aunt alisema suala hilo ni la kifamilia na kwamba yeye ndiye mwenye siri ya nani baba wa mtoto huku akishindwa kukubali kama ni Sunday Demonte ambaye ni mumewe wa ndoa, ndiye baba wa mwanaye Cookie.
“Mume wangu anapaswa anisikilize mimi, hakuna mahali niliwahi kusema kuwa mtoto huyu ni wa Iyobo (anayetajwa kuwa ni mpenzi wake), ni kweli nimepiga picha na Iyobo tukiwa na mtoto, lakini mtu yeyote anaweza kuja nyumbani, hata wewe (mwandishi), tukapiga picha nikiwa na mwanangu.
“Kuhusu Demonte, huyo ni mtu wangu, siwezi kusema mtoto ni wa kwake na siwezi kusema si wa kwake, ni mambo yangu binafsi, kama yeye (Demonte) akiamua kufuata maneno ya watu, sawa lakini ni bora anisikilize mimi mkewe,” alisema.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Aunt alimlalamikia mwandishi wetu kwa maswali mengi na mazito yaliyosababisha kukaukiwa maziwa kwenye matiti yake na kwamba kwa wakati ule hakujua mwanaye Cookie angenyonya nini.
“Ona sasa, umeniuliza maswali mengi hadi maziwa yamenikauka, sijui mwanangu atanyonya nini?” alilalamika Aunt.

0 comments:

-