Diva wa muziki wa Pop, Beyonce Knowles.
New York, MarekaniDIVA wa muziki wa Pop, Beyonce Knowles huenda akashika mimba hivi karibuni baada ya kuweka wazi kuwa yupo mbioni kupata mtoto wa pili na mumewe ambaye pia ni mwanamuziki wa Hip Hop, Shawn Carter ‘Jay-Z’.
Kwa mujibu wa Jarida la In Touch linaweka wazi kuwa Beyonce (33) ambaye ni mama wa mtoto mmoja, Blue Ivy (3), kwa miezi kadhaa yupo katika kutafuta mtoto mwingine lakini anachohofia ni malezi juu ya mtoto huyo ajaye.
“Kwa miezi miwili sasa anamtafuta mwanamke sahihi wa kuweza kumlea mtoto wake ajaye. Tayari wapo katika hatua za mwanzo na mumewe za kutafuta mtoto,” liliandika jarida hilo.
0 comments:
Post a Comment