Kim Kardashian ni
mwanadada ambaye anajulikana kwa kutengeneza headlines nyingi sana na
moja kati ya headlines anazoziweka public personality huyu ni zile
zinazohusu uzuri wake. Lakini Kim anasema
amechoshwa na fikra za watu wengi wanaodhani kuwa yeye ni mwanamke
mzuri tuu asiye na akili ya kufikria mbali, na kwa sababu hiyo staa huyu
ameweka headlines nyingine kubwa, ametangaza kurudi shule!
Kim Kadarshian amesema
anahisi yeye kama mtu binafsi hana uwezo mkubwa wa kutosha
kiakili. Licha ya mamillioni na umaarufu wote alionao sasa hivi, Kim
ameamua kurudi shule kupanua IQ huku akidai IQ yake haiko kwenye levo
anayoitaka na anaona bora arudi kusoma, ameshapata umaarufu na pesa yupo
tayari kuwekeza nguvu zake kwenye vitu vingine anavyoona ni muhimu na
mume wake Kanye West amekua akimsisitiza Kim kujaribu vitu tofauti haswa kipindi hiki ambacho ana mimba.
Lakini kumekuwa na baadhi ya watu wanaohisi kuwa jambo hili sio la ukweli na Kim anataka kupata watazamaji wengi zaidi wa Tv reality show yake Keeping up with The Kadarshians lakini msemaji wa
Kim amepinga maneno haya na kusema kuwa staa huyo yupo serious na
kurudi kusoma, na yeye kupata watazamaji wengi zaidi haiusiani ya
maamuzi yake binafsi. Kwenye interview aliofanya, staa huyo alisema;
>>> “Nahisi
nishafanikisha lengo la kuwa maarufu na tajiri, kwa kipindi cha zaidi
ya miaka kumi na kitu hilo ndio lilikua lengo langu, likatimia,
nikajulikana, nikawa tajiri, nikaolewa na kuzaa mtoto wangu wa kwanza na
sasa nategemea mtoto wa pili, nahisi umefika wakati wa mimi kurudi
kusoma”. >>> Kim Kadarshian.
Msemaji mkuu wa Kim Kadarshian amesema
kwa sasa wanaangalia namna ya kufanikisha zoezi la yeye kupata vipindi
maalum nyumbani kwake kwa ushirikiano wa mwalimu atakayekuwa tayari
kumsaidia kufanikisha lengo hili.
0 comments:
Post a Comment