Malaika
,Msanii anayetamba kwa sasa katika
game ya muziki wa tanzania na wimbo wake wa SARE amesema hivi karibuni video ya
wimbo wake huo unatarajiwa kuanza kuchezwa katika kituo kikubwa cha kimataifa
cha runinga
TRACE TV
Akizungumza
na MLIMANI TV malaika amesema walitakiwa wawe wametuma kazi hiyo lakini kuna
baadhi ya mambo ambayo uongozi wake unasubiri kuyakamilisha ili kuituma.
‘’Juzi
tulitakiwa tupeleke trace lakini bado tulikuwa hatujakamilisha kwa sababu wale
watu waliokuwa wametuandalia kwenye mfumo wa cd ilikuwa haijafika ukubwa wa
kwenda kule(trace)kucheza,kwa hiyo kwenye hizi wiki hizi,nafikiri management
yangu itasimamia ili kuweza kupeleka pia’’..alisema malaika
Ameongeza
pia kuwa video ya sare imeshaanza kuchezwa katika vituo vya televisheni vya
baadhi ya nchi za afrika ikiwemo bostwana.
Malaika
anasema wasanii wa kike wa Tanzania wanaofanya vizuri ni moja ya mambo
yanayomfanya kuendelea kukaza zaidi na hata kujitangaza kimataifa.
Mwanadada
huyu alianza kupata umaarufu kupitia katika wimbo wa chege USWAZI TAKE AWAY na
katika video ya wimbo huo na baadae akaja na wimbo wa MWANTUMU ambao
ulimtambulisha vema kwa mashabiki kabla ya kuja na huu unaotamba sasa SARE.
0 comments:
Post a Comment