RUBY BENDI ni bendi ya muziki wa kizazi kipya tanzania inayopatikana katika jiji la dar es salaam.band hii ya vijana wadogo wenye vipaji ni muungano wa wasanii wanne ambao ni ISMAIL YAHYA(SUMALAY),KHALID WAZIRI(KWEAPIPA),LAWRENCE CLEMENT(MAYA) NA SUNDAY MTOLE(C-MINOR).
Jina hili la Ruby Band linatokana na mmiliki wake Ruby Yusuph ambaye anamiliki kampuni ya Ruby International yenye studio ya RUBY RECODS na RUBY VIDEOS inayoshughulika na kurekodi nyimbo pamoja na kufanya video za nyimbo mbalimbali na filamu za kitanzania.
Mwezi june mwaka 2014 bendi hii
iliachia wimbo wao wa kwanza(audio) ulioitwa KISEBUSEBU wakimshirikisha msanii mwingine HANS WA LEO ambaye alikuwa akifanya kazi chini ya Ruby Records.
wimbo KISEBUSEBU ulifanya vizuri na kuwatambulisha vema vijana hawa katika tasnia ya muziki wa Tanzania wakiwa moja ya band chache za vijana wadogo wanaofanya muziki wa bongo flavour.mnamo septemba 27 2014 waliachia video ya wimbo huu ambao katika wiki yake ya kwanza tu baada ya kuwekwa youtube ulivuka zaidi ya watazamaji elfu 7.
mwezi January mwaka 2015 walitoa wimbo mwingine unaoitwa ‘NOMA’ambao uliweza kufanya vizuri zaidi na kuzidi kuwatambulisha vema kwa mashabiki wao.Tarehe 6mwezi machi walitoa video ya NOMA uzinduzi wake ukifanyika katika ukumbi wa ufukwe wa coco beach dar es salaam na watangazaji pamoja na wadau wa vituo vingi vya redio na TELEVISHENI vya dare s salaam.
Kuanzia hapo walizidi kufanya vema katika radio na vituo mbalimbali vya televisheni kote nchini. nyimbo nyingine walizowahi kutoa ni pamoja na KITU KIMOJA ambao unahamasisha kupiga vita mauaji ya albino yaliyoshamiri mwanzoni mwa mwaka 2015.Walitunga pia wimbo unaoitwa MWENGE wakati wakishiriki katika mbio za mwenge wa uhuru.
WASANII WANAOUNDA RUBY BAND
SUMALAY
ISMAIL YAHYA anafahamika zaidi kama SUMALAY .
huyu alitamba sana na wimbo wake ‘GAUNI LA KIJANI’
aliomshirikisha msanii aliyekuwa maarufu sana wakati
huo na sasa Matonya.
Wimbo huu ulifanya vizuri sana na kutamba katika vituo vingi vya redio hapa Tanzania.
alisoma masuala ya muziki katika chuo cha muziki maarufu kama nyumba ya vipaji
(Tanzania house of talent ) THT kabla ya kujiunga na Ruby Band.
KWEAPIPA
Jina lake halisi ni Khalid Waziri maarufu kama KWEAPIPA.Alianza talanta yake ya uimbaji katika chuo cha muziki maarufu kama nyumba ta vipaji Tanzania house of talent THT .Kabla ya kujiunga na Ruby Band alikua akifanya kazi kama solo artist .Alifanikiwa kurekodi wimbo mmoja ulioitwa SASAMBU ambao ulipata umaarufu kwa kiasi chake katika mitandao na radio mbalimbali nchini.
C-MINOR
Huyu ni mmoja wa waimbaji machachari wa Ruby Band akitokea IFAKARA mkoani Morogoro,Jina lake halisi ni SUNDAY MTOLE.Alikuwa akiimba katika matamasha mbalimbali mkoani morogoro .Aliweza kuwa na nyimbo kadhaa alizotunga lakini hazikuwahi kufika katika redio yoyote kwa wakati huo.
MAYA
Jina lake ni LAWRENCE CLEMENT lakini akiwa jukwaani anafahamika kama MAYA,Jina ambalo amekuwa akilitumia muda mrefu tangu alipoanza kujishughulisha na masuala ya muziki wa uimbaji huko IFAKARA MOROGORO.Aliwahi kutoa wimbo wake ‘ROHO INAUMA’ ambao ulifanya vizuri mkoani morogoro lakini haukuwa kufahamika sana nje ya mkoa.
UONGOZI WA RUBY BAND
RUBY BAND ipo chini ya Ruby International,kampuni inayojishughulisha na tasnia ya sanaa Tanzania na nje.Mmiliki wa kampuni hii ni mwanamama mfanyabiashara na mjasiria mali RUBY YUSUPH.
Katika Ruby International kuna RUBY RECORDS ambayo inajishughulisha na kurekodi muziki na nyimbo za wasanii mbalimbali.baadhi ya nyimbo ni kama ‘HIP HOP IS ALIVE’ wa Kalapina ft Qchilla,GOOD TIME wa Kalapina ft Ommy Dimpoz, Noma&Kisebusebu za Ruby Band na nyinginezo nyingi.
Pia kuna RUBY VIDEOS ambayo inashughulika na utengenezaji wa video za nyimbo za wasanii mbalimbali.baadhi ya video hizo ni pamoja na video kadhaa za MAPACHA WATATU ikiwemo YARABI NAFSI na SAUTI YA MAREHEMU ambayo ilishindanishwa katika tuzo za KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS.
Nyingine ni Kisebusebu na Noma zote za Ruby Band pamoja na THAMANI ya hans wa leo ft Amini na nyinginezo.
Kwa upande wa filamu ,RUBY VIDEOS imeshatengeneza filamu nyingi zikiwemo 'Baija' iliyoigizwa na wasanii maarufu kama MZEE MAJUTO,NIVA na wengine.Filamu nyingine ni NAJUTA KUPENDA iliyoigizwa na RIAMA ALLY,DAUDI DUMA(wa siri ya mtungi)KUPA,DEOGRATIUS SHIJA na wengineo.
0 comments:
Post a Comment