Kama wewe ni shabiki wa mastaa wowote wa mbele, basi utapenda kujua wana thamani ya kiasi gani cha pesa mwaka huu. Forbes imeachia orodha ya wasanii 100 wenye pesa zaidi kwa mwaka huu wa 2015, na kwenye orodha hiyo utakutana na watu kama Katy Perry, Beyonce, Kim Kadarshian, Floyd Mayweather, Manny Pacquiao, Taylor Swift na wengine kibao so unaweza ukavuta picha nani kampiku nani kwenye uwezo wa kifedha mwaka huu.
Staa anayeshika kijiti kwenye orodha ya mwaka huu ni Floyd “Money” Mayweather akiwa na thamani ya millioni $300 , Manny Pacquiao kwenye nafasi ya pili akiwa na thamani ya $160 million, Katy Perry akishika nafasi ya 3 akiwa na thamani ya millioni $130.
Kuonyesha uwezo wake wa kifedha, Floyd “Money” Mayweather kama wengi wanavyomuita ameamua kuweka headline juu ya headline, kaamua kununua gari jipya, gari lenye thamani ya millioni $4.8, aina ya Koenigsegg CCXR Trevita
gari ambalo kwenye rekodi ya dunia yapo matatu tu, na sasa akiwa mmoja
kati ya watatu wanaolimiliki gari hilo! Gari hilo litakuwa gari lake la
9,mengine nane yakiwa aina ya, Ferrarsi, Porsches, Lamborghinis, Bugattis na ndege yake binafi aina ya Gulfstream V private jet vyote hivi vikiwa na thamani ya millioni $55.
Hapa chini nimekusogezea orodha ya mastaa kumi tuu kutoka kwenye list ya Forbes 100 Richest Celebrities 2015, pamoja na picha ya gari jipya la Floyd Mayweather pamoja na picha inayo onyesha jumla ya magari alionayo na ndege yake.
1. Floyd Mayweather ($300 million)
2. Manny Pacquiao ($160 million)
3. Katy Perry ($130 million)
4. One Direction ($130 million)
5. Howard Stern ($95 million)
6. Garth Brooks ($90 million)
7. James Patterson ($89 million)
8. Robert Downey Jr. ($80 million)
9. Taylor Swift ($80 million)
10. Cristiano Ronaldo ($79.5 million)
0 comments:
Post a Comment