Tuesday, November 10


Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ametoa ushauri wake kwa kiongozi mkuu wa nchi ili kuleta mabadiliko makubwa katika mfumo.
 
Zitto ameandika kupitia ukurasa wake wa Facebook, japo hakutaja jina lakini maelezo yake yanaonesha kuwa mwenye uwezo wa kufanya maamuzi hayo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, ndiye mlengwa wa ujumbe huo.
 
Hivi ndivyo alivyoandika:
“Thomas Sankara once said “You cannot carry out fundamental change without a certain amount of madness”. Uwendawazimu 
 
1) Weka mikataba yote ya Rasilimali za Nchi wazi – PSAs and MDAs 2) Futa posho za makalio katika mfumo mzima wa Serikali kama Mpango wa Maendeleo unavyotaka 
 
3) Futa business class air tickets Kwa watendaji wa Serikali na wanasiasa isipokuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu

 4)Futa matumizi ya mashangingi ( BoT wameonyesha mfano kwenye hili ) 
 
5 )Futa uagizaji wa sukari kutoka Nje na anzisha miradi ya miwa tuuze sukari Nje 
 
6 )Weka wazi taarifa ya Serikali kuhusu utoroshaji wa fedha na fungua mashtaka Kwa wahusika mara moja 
 
7 )Wape takukuru mamlaka ya kukamata na kushtaki na kila mwenye Mali athibitishe yeye kaipataje (reverse burden of proof ) 
 
8 )Mali na Madeni ya Viongozi yawe wazi Kwa umma na wananchi waruhusiwe kuhoji 
 
9 )Ruhusu mshindi wa uchaguzi Zanzibar atangazwe na ufanye naye kazi 
 
10)Acha mchakato wa Katiba Kwa kuanzia alipoishia Warioba, achana na Katiba Pendekezwa.”

0 comments:

-