Aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Frederick Mwakalebela amefungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Iringa mjini yaliyompa ushindi Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema huku akiitaja kofia ya M4C katika shtaka lake.
Msajili
msaidizi wa mahakama kuu ya kanda ya Iringa , Ruth Massama amesema kuwa
Mwakalebela alifungua shtaka hilo mahakamani hapo Oktoba 30 mwaka huu.
Katika
shitaka hilo, pamoja na mambo mengine, Mwakalebela anamtuhumu Msigwa
kwa kuvunja sheria ya uchaguzi kwa kuvaa kofia yenye nembo ya M4C
inayotumiwa na Chadema, katika siku ya kupiga kura.
Kadhalika,
mlalamikaji huyo anamtuhumu mwangalizi wa uchaguzi kwa kukiuka sheria
na kanuni za uchaguzi wakati wa zoezi la kupiga na kuhesabu kura.
Katika
madai yake, Mwakalebela ameeleza kuwa katika kata ya DaboDabo
alikataliwa kuingia katika kituo cha kupigia kura wakati wakati
mshindani wake huyo aliruhusiwa kuingia bila kizuizi chochote.
Msimamizi
wa uchaguzi katika jimbo la Iringa Mjini alimtangaza Mchungaji Peter
Msigwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo hivyo kupata nafasi ya kuendelea
kuliwakilisha jimbo hilo kwa muhula wa pili.
0 comments:
Post a Comment