Tuesday, November 10


Justin Bieber.
KAMA wewe ni mdau wa burudani, Jina la JUSTIN BIEBER linaweza lisiwe geni masikioni mwako hasa kutokana na umaarufu mkubwa alioupata kupitia kipaji chake cha uimbaji tangu akiwa kijana mdogo.
Bieber aliyeanza kutambulika mwaka 2008 akiwa na miaka 14 na kujulikana zaidi kupitia kibao chake cha Baby alichomshirikisha mkali wa Hip Hop,Ludacris, ameweza kuwa mmoja kati ya wasanii wenye umri mdogo wanaoingiza mkwanja wa kutosha kupitia muziki wake huku mafanikio yake yakitumika kama mfano wa vijana wengine wanaochipukia kwenye tasnia hiyo.

Hata hivyo, wakati staa huyo akizidi kujipatia mafanikio, mashabiki wake wengi waliokuwa wakimchukulia kama mfano wa kuigwa wamembadilikia kwa kumuona kama mtu asiyefaa kuigwa na jamii hasa watoto wadogo kutokana na vituko anavyovifanya kila kukicha visivyoendana na maadili ya nchi nyingi hasa za Kiafrika.
Kwa mujibu wa wasifu wake, Justin Bieber anatajwa kukulia katika maadili ya Kikristo na familia ya kawaida kabla ya kuukwaa umaarufu wa ghafla kupitia nyimbo zake ambapo staa huyo amebadilika kabisa huku kila mara akiripotiwa kwenye vyombo vya habari kwa kufanya vituko vya kila aina vinavyoonesha jinsi gani amekengeuka tofauti na malezi aliyokulia.
Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya burudani wamekuwa wakimtolea mfano Bieber kama mwathirika wa mambo matatu ambayo ni; umaarufu uliopindukia na pesa nyingi tofauti na umri wake vitu ambavyo kwa pamoja ni hatari kwa msanii kama yeye kwa kuwa ni rahisi kuingia katika tabia hatarishi kama matumizi ya madawa ya kulevya na tabia nyingine za ajabu.Vifuatavyo ni baadhi ya vituko vya staa huyo:
Adakwa akivuta bangi Januari 2, mwaka 2013 Bieber alidakwa kwa shutuma za kuvuta bangi na kunywa vilevi ndani ya chumba cha hoteli iliyomo ndani ya Ufukwe wa Newport, Marekani pamoja na rafiki yake mkubwa Lil Twist, hata hivyo baadaye aliachiwa huru.
Baada ya tukio hilo Bieber aliachia Kibao cha To Be Better chenye maudhui ya kuwaomba msamaha mashabiki wake kwa kitendo hicho.
Ampiga paparazi Akiendeleza mnyororo wa vituko vyake Bieber amewahi kuingia katika skendo iliyomchafua zaidi baada ya kumchapa kibao paparazi huko London alipomfuata kwa lengo la kumpiga picha, hata hivyo baada ya paparazi huyo kucharuka, Bieber aliingia ndani ya gari lake na kutokomea huku akiporomosha matusi.
Ajisaidia haja ndogo kwenye ndoo ya kupigia deki hotelini Kati ya vituko vya Bieber vilivyowahi kuwashangaza wengi ni kile cha kujisaidia haja ndogo kwenye ndoo ya kupigia deki katika chumba cha kulala wageni kwenye hoteli moja maarufu jijini New York, sambamba na kusambaza picha akifanya tukio hilo huku akimtukana aliyewahi kuwa Rais wa Marekani, Bill Clinton. Hata hivyo, taarifa baadaye zilidai dogo huyo alifanya hayo akiwa amelewa.
Atangaza kuacha muziki Mwishoni mwa mwaka 2014, Bieber aliwaacha midomo wazi wapenzi wake baada ya kutangaza kuacha rasmi muziki. Baada ya kuposti taarifa hiyo kwenye mtandao wake wa Twitter mashabiki wake walimjia juu kwa kumponda lakini baadaye alipofanya mahojiano na gazeti la kila siku la New York alidai kuwa taarifa hizo alizitoa kama utani.
Anunua machangudoa Iliwahi kuripotiwa alipokuwa kwenye ‘tour’ nchini Brazil,Bieber alichepuka kwa kumsaliti aliyekuwa mpenzi wake Selena Gomez baada ya kwenda kutalii kwenye mji wa Rio de Janeiro
alikoibuka na machagudoa wawili ambao alirudi nao hadi hotelini.

0 comments:

-