Mkongwe wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma yake ya For You, Abubakari Katwila ‘Q Chillah’.
Mkongwe wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma yake ya For You, Abubakari
Katwila ‘Q Chillah’ amefunguka kuwa ukubwa wa jina lake ndiyo
umemrudisha kwenye gemu kwa kasi na kumfanya ajitume sana kufanya muziki
wake.kizungumza na paparazi wetu, Q Chillah alisema kuwa katika kipindi alichokuwa kimya aligundua kuwa watu wengi walikuwa wakimiss kazi zake jambo ambalo lilimfanya agundue ukubwa wa jina lake hivyo kuamua kupambana kwenye muziki ili arudishe heshima aliyojitengenezea siku za nyuma.
“Niligundua jina nililojitengenezea kwenye muziki ni kubwa mno hivyo kwa njia yoyote ilikuwa lazima nirudi na nifanye kazi kubwa kama nilivyozoeleka. Kwa sasa nipo kikazi zaidi ,” alisema Q Chillah.
0 comments:
Post a Comment