Kaimu IGP, Abdallah Kaniki akiwa kwenye mkutano huo.
Na Haruni Sanchawa / GPL
Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji
Damiani Lubuva leo ametoa wito kwa vyama vya siasa kwamba siku ya
uchaguzi mkuu baada ya mpigakura kutimiza haki yake aondoke eneo la
kituo cha kupigia kura laa sivyo sheria itachukua mkondo wake.
Kiongozi huyo aliyasema hayo alipokuwa
katika mkutano na viongozi wa vyama vya siasa katika Hoteli ya New
Afrika jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa, tume inaongozwa kwa sheria na
kila agizo linalotolewa ni kwa mujibu wa sheria hivyo ni vyema viongozi
hao wakatii na kuhakikisha wanawapa taarifa wafuasi wao kwamba
wakishapiga kura warudi makwao.
Aliongeza kuwa ile dhana ya kwamba baada ya
kupiga kura wanachama wabaki kulinda kura ni kinyume na sheria kwani
wenye jukumu la kufanya hivyo ni vyombo vya dola.
Naye Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi
Tanzania, Abdallah Kaniki amesisitiza kuwa jeshi la polisi limejipanga
vya kutosha kuhakikisha siku ya kupiga kura zoezi linafanyika kwa amani
na umakini wa hali ya juu.
Kaniki alisema kwamba kazi ya usalama viachiwe vyombo vya ulinzi na usalama na si mtu binafsi au kikundi flani.
Akasisitiza kuwa atakayekwenda kinyume na
maagizo ya tume hatua kali zitachukuliwa na hakuna suala la lelemama
kwani kinachotakiwa ni haki pamoja na amani.
0 comments:
Post a Comment