Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,
Paul Makonda (kulia), akihutubia wananchi baada ya kupokea matembezi ya
amani ya vyama vya siasa yaliyofanyika kuanzia eneo la Magomeni hadi
viwanja vya Kinondoni Biafra Dar es Salaam leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Wilaya ya Chama cha Union For Multi Party Democratic (UMD), Abdallah Tumbo akihutubia katika mkutano huo.
Katibu wa Wilaya ya Kinondoni wa Chama cha UDP, Makoye Ikoles, akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Wilaya wa Chama cha UPDD, Salim Choya akizungumza katika mkutano huo.
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Kinondoni, Athuman Shesha akihutubia katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani
wa dini zote Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum, akiongoza
dua za kuombea nchi amani katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani wa dini zote Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni katika mkutano huo.
Dua la kuombea taifa ikiendelea.
Vijana wa Joging wakishiriki matembezi hayo.
Matembezi yakiendelea.
DC Makonda (katikati), akiwa na Viongozi wa vyama vya siasa walioshiriki maandamano hayo.
Vijana wa Jogging wakiwa jukwaa kuu wakiimba wimbo maalumu wa amani.
Na Dotto Mwaibale
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda amesema kila mtu ana
wajibu wa kuilinda na kudumisha amani iliyodumishwa na waasisi wa nchi
hii hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika
Oktoba 25 mwaka huu.
Makonda alitoa mwito huo wakati akihutubia wananchi baada ya
kupokea matembezi ya kuombea nchi amani yaliyofanyika katika viwanja vya
Biafra Dar es Salaam leo.
Maandamano hayo yameratibiwa na Makonda katika wilaya yake kwa niaba ya watanzania wote.
Makonda alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zilizodumu kwa
amani na amani hiyo ilidumishwa na waasisi wa Taifa hivyo imebaki kuwa
kimbilio na tegemeo kwa watanzania.
Alisema ili kuwaenzi waasisi hao ni kutunza tunu hiyo na kwamba
yapo mataifa yamepita katika nyakati mbalimbali za uchaguzi lakini
hawana amani kama tuliyonayo hivyo tuna wajibu mkubwa kuitunza.
"Vipo viashiria vya uvunjifu wa amani, lakini ikumbukw kuwa amani
ni kubwa kuliko ahadi za mgombea yoyote wa chama cha siasa hivyo hakuna
kinachoweza kufanywa na mgombea yeyote kama hakuna amani,"alisema.
Hata hivyo Makonda alisema kuwa aliandika barua kwa kila chama cha
siasa ambapo vyote vilithibitisha kushiriki lakini cha kushangaza baadhi
havijahudhuria kwa kutoa sababu zisizo na msingi wowote kama kutokuwa
na nauli na mambo mengine.
"Niliviandikia barua vyama vyote, lakini vingine havijahudhuria kwa
makusudi hivyo dalili mnayoona hapa ni dalili tosha kuwa amani
wanayohubiri kwenye majukwaa si hii wanayoitaka,"alisema Makonda.
Makonda aliongeza kuwa vyama vilivyoshiriki katika maandamano hayo
ya amani ni CCM, CUF, UPDP, UDP,UMD, Jahazi asilia na vilabu vya Jogging
.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa
wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum alisema mtu yeyote asiyependa
amani ni adui wa Mungu.
Sheikh Alhad aliitoa kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam leo wakati
alipoongoza dua maalum ya kuombea amani wakati wa maandamano ya vyama
vya siasa yaliyofanyika kuanzia eneo la Magomeni hadi viwanja vya
Kinondoni Biafra.
Alisema kuwa anavipongeza vyama vilivyothibitisha kushiriki
maandamano hayo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Konondoni, Paul Makonda na
kamati ya ulinzi kwa kuandaa shughuli hiyo.
Alisema kuwa kuna baadhi ya vyama ambavyo vilitakiwa kushiriki
lakini havijashiriki ambapo havijaathiri chochote na kuweka wazi kuwa
wachache wanaweza kufanya mambo kwa ajili ya wengi.
"Kuna baadhi ya vyama havijashiriki maandamano haya, hivyo
vikumbuke kuwa watu wachache wanaweza kufanya mambo kwa ajili ya wengi
hivyo ni jambo kubwa na kwamba mungu analisikia,"alisema.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya viongozi na wawalikishi
wa vyama hivyo walisema kuwa watanzania wanapaswa kupiga kura kwa amani
pia walishamaliza wakatulie nyumbani kusubiri matokeo kutoka kwa
mawakala wanaowaamini waliowaweka vituoni.
0 comments:
Post a Comment