Picha mbali mbali za wajumbe na viongozi na wataalamu (washauri) kutoka shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) pamoja na wafanyakazi wa Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania wakiwa katika semina ya juu ya usimamizi wa sheria na kanuni za usimamizi wa mionzi ya nyuklia Tanzania, iliyofanyika makao makuu ya Tume ya Mionzi Tanzania yaliyopo jijini Arusha. Picha na Yohana Challe.</ span> |
NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), imesema kuwa
imejiandaa vilivyo katika usimamizi wa uchimbaji wa madini ya urani ambayo
yanapatikana kwa wingi hapa nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia
John Mngodo alisema kuwa moja ya
majukumu ambayo serikali inafanya ni kujiandaa juu ya kusimamia uchimbajia wa
madini hayo.
“Mkazo uliowekwa hapa ni kwamba ni lazima usalama wa mionzi upewe
mkazo hivyo TAEC itahakikisha usalama unakuwepo na katika kila hatua ambayo
watakuwa wanajiandaa au wanachimba na kusafirisha madini ya urani lazima ukaguzi
ufanyike na kutoa kibali ili kuhakikisha usalama unakuwepo” alisema Mngodo.
Mngodo alizungumza hayo wakati wa kuhitimisha zoezi la
kupitia taratibu za uendeshaji, ukaguzi na usimamzi wa nyuklia na mionzi hapa
nchini, zoezi hili lilifanyika kwa siku kumi tangu Oktoba 4 hadi oktoba 14 mwaka
huu katika makao makuu ya Tume hiyo mkoani hapa kwa kushirikiana na wataalamu kutoka
zaidi ya nchi 10 duniani.
“Wataalamu hawa walikuwa wakipitia taratibu na namna ya jinsi
ambavyo tunavyosimamia shughuli za mionzi na nyuklia hapa nchini” alisema
Mngodo.
Wataalamu hawa wametokea katika nchi za Jordani, Irend,
Ubelgiji, Sudani, Kenya,Ukreini, Argentina, Australia, Pakistani, Nigeria,
Zimbabwe, Uingereza na Zambia
Wataalamu hawa walikuja kwa mwaliko wa serikali ili kuweza
kuisaidia Tume hii ili kuweza kuboresha zaidi shughuli zinazoendelea hasa elimu
kwa wafanyakazi, pamoja na kupitia sheria na kanuni za usimamizi wa masuala ya
Nyuklia na mionzi hapa nchini.
Aliongeza kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni jinsi
ya kuwapata wataalamu wa kusimamia shughuli hizo (rasilimali watu) pamoja na
fedha, japo akiipongeza serikali kwa kuendelea kujitahidi kutoa mafungu ili
kuendelea kuboresha shughuli za Tume.
Kwa upande wake Leonard Kifanga ambaye ni Mwanasayansi
mwandamizi wa nyuklia, alisema kuwa
lazima Tanzania iwe na mipango mikakati ya kuboresha na kushughulikia ajali za
kinyuklia zinazoweza kujitokeza, kwani itasaidia kujiepusha na madhara ambayo
yanaweza kuepukika kwa urahisi na kwa haraka.
“Nashauri lazima Tume na Taasisi za kusimamia majanga ziwe
huru ili zifanye kazi kwa uhuru zaidi na kwa haraka ili kila mtu aweze
kuwajibika katika nafasi yake na hii itasaidia kujua tatizo lilipoanzia”
alisema Bwana Kifanga.
0 comments:
Post a Comment