Kuna kipindi Chris Brown aliweka headlines za kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaweke wawili, Rihanna na Karrueche Tran kwa wakati mmoja, na mwishoni wa mwaka 2012 msanii huyo alionekena pande za Australia na Karrueche akispend Christmas na siku ya Valentine tarehe 14 February ya mwaka 2013 Chris alionekana Marekani na staa wa muziki wa R&B Pop Rihanna!
Nimekutana na interview moja ambayo Chris Brown alishawahi kufanya na humo ndani staa huyo alizungumza kitu ambacho sikuwahi kukijua… Chris alifunguka kuhusu kuwa kwenye mahusiano na wanawake wawili aliowapenda sana, ila kikubwa zaidi alichokigusia Chris ni issue ya Karrueche Tran na Rihanna kukutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza kwenye moja ya party aliyokuepo… ilikuaje?! Chris Brown aliisogeza stori kama hivi..
>>> “Kuna
kipindi nilienda nje ya nchi nadhani ilikuwa ni Cannes, na ilikuwa ni
kipindi ambacho nilikuwa na mpenzi lakini bado ninaongea na kuwasiliana
na Rihanna… so nilienda huko kwa ajili ya kushoot video, badaae
wakarusha bonge la party kwenye boti na girlfriend wangu alikuwepo, na
kama dakika 15 badaae Rihanna akaja nikasema mungu wangu hapa
nitafanyaje!!… Lakini unajua nini walikuwa poa wenyewe, wakasalimiana
vizuri japo nilikuwa naombaa sana wasiparuane, nilikuwa naomba sana… ila
walikuwa wastaarabu sana na hiyo ndio siku ambayo nilijua wananipenda…” <<< Chris Brown.
0 comments:
Post a Comment