Thursday, October 15

Mkazi wa Arusha na mpenzi wa bia ya Serengeti Premium Lager Laota Elias akishiriki katika shindano la mwisho la kumtafuta Serengeti Masta wa jumla kwa mkoa wa Arusha katika kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager. Mashindano hayo ya mwisho yalifanyika katika baa ya Bondeni iliyopo Kijenge juu jijini Arusha ambapo yaliwakutanisha washindi mbalimbali wa baa za mkoa huo waliofika kuchuana vikali ili kumpata mshindi wa jumla. Kampeni hiyo imefikia tamati jijini humo baada ya kudumu kwa takribani miezi miwili ikizunguka baa kwa baa kusaka washindi waliopewa jina la “Serengeti Masta”.

Mkazi wa Arusha Cleophas John akifurahi pamoja na marafiki zake baada ya kupita kwenye ngazi ya kwanza ya shindano la kumtafuta “Serengeti Masta” wa mkoa wa Arusha linaloendeshwa na bia ya Serengeti Premium Lager toka SBL wakati wa  shindano hilo ambalo lilifanyika katika baa ya Bondeni-Kijenge juu jijini Arusha. Shindano hilo limefikia tamati jijini humo baada ya kudumu kwa takriban miezi miwili (2) ikiwaburudisha na kuwazawadia wateja wa bia hiyo na kuwafundisha wahudumu wa baa mbalimbali juu ya utoaji huduma kwa wateja

Mratibu wa mashindano ya kumsaka Serengeti Masta Yassin Khalfan (katikati) akiwa na baadhi ya washiriki wa shindano hilo kutoka Baa mbalimbali jijini Mbeya kushoto ni Faraji Mbwambo kutoka Gambino Bar na Ibrahim Allan kutoka Liz Pub. Kampeni hiyo ya Serengeti Masta imewakutanisha wateja na mameneja wa bia hiyo katika kujifunza kwa undani kuhusiana na bia ya Serengeti Premium Lager ambapo mameneja hao walitoa zawadi mbalimbali kwa washindi walioweza kuitambua ladha halisi ya bia hiyo katika kipindi chote cha kampeni ambapo pia waliweza kuwafikia wahudumu wa baa zaidi ya 4000 katika miji tofauti.

Mshiriki wa shindano la Serengeti Masta na mkazi wa Arusha Daniel Mwakasungule akionja ladha tofauti za bia zilizo mbele ya meza yake ili kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager katika shindano la kumpata Serengeti Masta wa mkoa wa Arusha ambalo lilifanyika katika Baa ya Bondeni, Kijenge juu jijini Arusha mwishoni mwa wiki hii.

Mshindi wa jumla wa shindano Serengeti Masta kwa jiji la Mbeya Faraji Mbwambo kutoka baa ya Gambino jijini Mbeya akionesha kitita cha fedha sh. 100,000 alizotunukiwa baada kuibuka mshindi wa jumla wa kuitambua ladha ya bia ya Serengeti Premium Lager kati ya vinywaji vitano vinavyozalishwa na kampuni ya SBL. Kampeni hiyo ya Serengeti Masta imewakutanisha wateja na mameneja wa bia hiyo katika kujifunza kwa undani kuhusiana na bia hiyo ambapo mameneja hao walitoa zawadi mbalimbali kwa washindi walioweza kuitambua ladha halisi ya bia hiyo katika kipindi cha kampeni
Mmoja wa wateja na mnywaji maarufu wa bia ya Serengeti Premium Lager Tuntufye Mwakaje maarufu kwa jina la “Tupac” akiburudika na bia hiyo wakati wa shindano la kumsaka Serengeti Masta wa jumla kwa wakazi wa jiji la Mbeya lililofanyika  kwenye baa ya Mbeya Pazuri.

0 comments:

-