Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
'Diamond Platnumz' baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere akitokea nchini Marekani alipotwaa tuzo tatu za Afrimma.
Diamond akiwa na tuzo zake akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) muda mfupi baada ya kutua uwanja wa ndege.
Diamond akianza safari ya kuelekea Escape One kutoka uwanjani hapo.
Akiwa barabarani kuelekea Escape One.
Bodaboda wakiongoza msafara wa Diamond kuelekea Escape One.
Diamond akizidi kukatiza mitaa mbalimbali ya jiji la Dar.
Mashabiki wakia katika msafara wa Diamond.
Diamond akiongea na mashabiki wake njiani wakati akielekea Escape One.
MWANAMUZIKI nguli wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul 'Diamond Platnumz' leo amepokelewa kwa shangwe na mamia ya
mashabiki wake waliohudhuria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Diamond ametua nchini akitokea Marekani
alipokwenda kwa ajili ya zoezi la utoaji tuzo za Afrimma ambapo alitwaa
jumla ya tuzo tatu.
Baada ya mapokezi hayo Diamond akiwa na
msafara wa mashabiki wake walielekea Escape One, Mikocheni kwa ajili ya
kuzungumza na wanahabari pamoja na kupiga picha za pamoja na mashabiki
wake.
(PICHA NA MUSA MATEJA / GPL)
0 comments:
Post a Comment