Thursday, October 15

phone (2)
Picha ya kipimo cha X-ray ikionesha simu na chaja zikiwa zimesagwasagwa ndani ya tumbo la mfungwa huyo.
phone (3)
Simu na chaja alizomeza mfungwa huyo.
phone (1)
Mfungwa akitoka kusalimia ndugu na jamaa zake.
MFUNGWA mmoja (hakufahamika jina lake) nchini Brazil amemeza simu ya mkononi na chaja zake mbili wakati akijihami na kukataa kuingizwa gereza la Papunda liliyopo mji mkuu wa nchi hiyo, Brasilia.
Tukio hilo lilitokea juzi wakati mfungwa huyo na wengine waliporuhusiwa kwenda kutembelea ndugu na jamaa zao wakati wa Siku ya Watoto nchini Brazil ambayo inasherehekewa na familia nyingi zaidi nchini humo kuliko sikukuu yeyote kiutamaduni na kiuchumi. Siku hiyo watoto hupewa zawadi mbalimbali na wanafamilia wao.
Vipimo vya mionzi kwa njia ya X-rays vimeonesha kuwa simu na chaja hizo tayari vimeharibu vibaya sehemu ya utumbo wake,  juhudi mbadala za kuweza kunusuru maisha yake zimeendelea kufanywa na madaktari. Taarifa zaidi zinasema kuwa mbali na mtuhumiwa kutenda tukio hilo, amerudishwa rumande japo haijafahamika hapo mwanzo alikuwa amefungwa kwa kosa gani.
Gavana wa gereza hilo amesema kuwa mfungwa huyo atapoteza haki za msingi alizokuwa nazo hapo mwanzoni na sasa atapewa adhabu kwa kosa jipya alilofanya la kumeza simu ya mkononi na chaja. Mnamo Agosti 11, 2000 wafungwa watano walifariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa wakati  askari wakituliza ghasia kwenye gereza hilo la Papuda ambapo Oktoba 2001 watu wawili walikufa na wengine 11 kujeruhiwa kwenye tukio kama hilo.

0 comments:

-