Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kada wa CCM, Balozi Juma Mwapachu leo amerudisha kadi ya uanachama katika ofisi za CCM Kata ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Amesema
anajiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kwamba baada ya
Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 atatangaza chama anachojiunga miongoni mwa
Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD vinavyounda umoja huo.
Mwapachu
amesema haoni sababu ya kutaja chama hicho sasa kwa vile lililo muhimu
kwao hivi sasa ni umoja miongoni mwa wanamabadiliko na kujipambanua
katika imani ya chama cha siasa hakuwezi kuwa na tija kwa umoja huo.
Amesema
Lowassa anakwenda kuwa Rais wa Wanaukawa wote, hivyo watu wote
wanaoamini katika mabadiliko ndani ya vyama hivyo wanapaswa kuwa wamoja
kwa kuuwezesha umoja huo kuibuka na ushindi.
Akizungumza
baada ya zoezi hilo, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mtaa wa Mikocheni
A, Sudi Odemba amesema chama chake hakitapata madhara yoyote kutokana
na hatua ya Balozi Mwapachu kijiengua na kutangaza kujiunga Ukawa.
Amesema
Mwapachu hakuwa mwanachama aliyejitoa kukisaidia chama katika siku za
karibuni na kwamba hajawahi kushiriki mikakati thabiti ya kukipatia CCM
ushindi katika ngazi ya mtaa japo chama hicho kiliweza kuibuka na
ushindi wa kishindo.
Jumanne
wiki hii, Balozi Mwapachu alitangaza kujitoa CCM akikituhumu kukiuka
misingi ya kidemokrasia wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais
Julai mwaka huu ambapo Dk John Magufuli alichaguliwa huku mgombea
anayeamini kuwa na maono ya kiuongozi kwa Tanzania ijayo, Edward Lowassa
akikatwa.
0 comments:
Post a Comment