Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwamuru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima awasilishe Mahakamani hapo vyeti vinavyoonesha kuwa ni mgonjwa.
Amri
hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha
baada ya Gwajima kushindwa kufika mahakamani kwa ajili ya usikilizwaji
wa kesi inayomkabili.
Gwajima
anakabiliwa na kesi ya kutumia lugha chafu dhidi ya Akofu Mkuu wa
Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinal
Pengo.
Kesi
hiyo ambayo tayari imeshaanza kusikilizwa ilitarajiwa kuendelea
kusikilizwa mahakamani hapo ambapo upande wa mashtaka ulitarajiwa
kuwasilisha kielelezo cha ushahidi ambacho ni mkanda wa video unaodaiwa
kumwonesha Gwajima akitoa lugha hiyo chafu dhidi ya Kardinal Pengo.
Hata
hivyo Gwajima hakutokea mahakamani na badala yake, Wakili wake Peter
Kibatala aliieleza mahakama kuwa mteja wake hakuweza kufika mahakamani
kwa kuwa anaumwa. Hata hivyo haikuweza kubainishwa kuwa Gwajima anaumwa
nini.
Wakili
wa Serikali Lilian Itemba aliiomba mahakama iagize mshtakiwa huyo
awasilishe mahakamani vyeti vinavyothibitisha kuwa anaumwa.
Hakimu
Mkeha alikubaliana na ombi hilo la upande wa Serikali na kuamuru
mshtakiwa huyo awasilishe mahakamani hapo vyeti hivyo, siku ya tarehe ya
kuendelea kwa usikilizwaji wa kesi hiyo.Hakimu Mkeha aliahirisha kesi
hiyo hadi Novemba 4, 2015.
0 comments:
Post a Comment