Staa anayesumbua kwa sasa na Kibao cha Shauri Zao, Abedinego Damian ‘Belle 9’.
STAA anayesumbua kwa sasa na Kibao cha Shauri Zao, Abedinego Damian ‘Belle 9’ amefunguka kuwa kufuatia wimbo wake huo kuanza kufanya vizuri kimataifa ikiwa ni pamoja na kuchezwa kwenye vituo mbalimbali vya televisheni ikiwemo Trace Urban kumemfanya apate mzuka wa kuandaa kazi nyingine kali ambayo anategemea itamfikisha kimataifa zaidi ya hapo alipo.
Akichonga na Centre Spread, Belle alisema hatua hiyo aliyopiga kwa sasa anadhani ndiyo ambayo mashabiki wake walikuwa wanaililia aifikie na kwa kuwaheshimu mchango wao atahakikisha ana washa moto ambao hauzimiki ili kufika mbali zaidi.
“Kila mara nilikuwa napenda kusema kuwa wakati wangu haujafika lakini sasa nathubutu kusema it’s my time to shine na moto ninaokwenda kuuwasha kwa kazi zinazofuata hakuna wa kuuzima,mashabiki zangu wategemee vitu vikubwa sana,” alimaliza Belle.
0 comments:
Post a Comment