"Tutajenga
nidhamu ya matumizi ya serikali na kuachana na matumizi yasiyo na
msingi ambayo yamekuwa utamaduni kwenye serikali ya sasa. Kwa mfano,
Magari ya kifahari, safari zisizo na tija, posho zisizoeleweka, semina
na makongamano yasiyoisha. Vyote hivi vitafikia ukomo".
"Tutapunguza misamaha ya kodi kufikia asilimia moja (1%) tu ya pato la taifa (au chini ya hapo) kama inavyoshauriwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Wenzetu Kenya na Uganda wameweza. Tanzania inapoteza zaidi ya Shilingi trilioni moja nukta nne kila Mwaka kutokana na misamaha holela ya kodi.
- Tukilitekeleza hili pekee, tutaweza kulipa Deni la Walimu la Shillingi Bilioni Thelathini na Tatu na bado chenji kubwa ikabaki kuboresha maslahi ya Polisi, Madaktari, n.k.
- Kwa mujibu wa Wizara ya Fedha, kiasi cha misamaha ya kodi katika mwaka wa fedha 2014/15 kilikuwa Shilingi Trilioni 1.419. Katika kipindi hicho, serikali ilitegemea kukusanya takriban Shilingi Trilioni 10 kama kodi. Hii inaonyesha kwamba kiasi cha misamaha kilikuwa asilimia 14 ya mapato ya kodi.
Kuhakikisha kwamba misamaha yote ya kodi inawekwa wazi na inakaguliwa na mamlaka ya kodi (TRA), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha Za Serikali (CAG), pamoja na Kamati husika za Bunge".
"Tutaongeza makusanyo ya mapato ya ndani kutoka Asilimia Kumi Na Tano (15%) ya pato la taifa na kufikia Asilimia Ishirini kama wenzetu Kenya n.k.
Tutadhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu wanaotumia vibaya mfumo wa kodi kutoa mizigo yao bandarini.
Tutahakikisha kwamba Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) inakagua gharama za uwekezaji zinazofanywa na makampuni ya nje ili kutoza kodi sahihi. Udanganyifu wa baadhi ya makampuni husababisha upotevu wa mapato ya serikali".
"Tutahakikisha kwamba mikoa mingine ya nchi yetu inachangia zaidi kwenye makusanyo ya kodi. Kwa sasa asilimia 70 ya mapato yanayokusanywa na TRA yanatoka Dar es Salaam.
Tutaongeza idadi ya walipa kodi kwa kuja na sheria mpya ambayo itahakikisha kwamba kila Mtanzania anayefikisha umri wa miaka kumi na nane anasajiliwa kama mlipa kodi na kama ana shughuli ya kumuingizia kipato, analipa kodi inayostahili bila kuonewa.
Tutaboresha mfumo wa kodi kwa lengo la kuwawezesha wananchi waone faida ya kulipa kodi kwa kuwapatia huduma za kijamii zinazoendana na kodi wanazotozwa."-Edward Ngoyai Lowassa

0 comments:
Post a Comment