Ripoti kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu ni
kama hazisikiki sana sasahivi kutokana na jinsi ambavyo Siasa imeteka
Headlines za Vyombo vya Habari, lakini taarifa ikufikie kwamba Ugonjwa
huo bado upo Dar es Salaam.. wapo wanaoendelea kufariki, wapo wanaopata
maambukizi na wapo pia waliolazwa na wanaendelea kutibiwa Hospitali.
Leo October 12 2015
ninayo Ripoti ya kingine kinachoendelea katika Manispaa ya Kinondoni
kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu… Hii imetolewa na Afisa Afya wa Manispaa,
Mathias Kapizo >>>>”Mpaka sasahivi tuna wagonjwa wapya 35… Wagonjwa
35 katika Wilaya kama Kinondoni ni watu wengi… Sehemu kubwa
zilizoathiriwa na Kipindupindu kwa sasa ni Manzese, Tandale, Mabibo,
Makurumla, Mburahati, Kigogo, Mwananyamala, Magomeni Sinza, Makumbusho
na Kijitonyama.”
“Bahati
mbaya tumepoteza watu 12 mpaka sasa kwa ugonjwa wa Kipindupindu… Kwa
mujibu wa taarifa ya tarehe 12 jumla ya wagonjwa wote waliougua
kipindupindu tangu kilipoanza tarehe 15 mwezi wa nane wanafikia 1564 kwa sasa…“- Mathias Kapizo.
Kuhusu idadi ya Wagonjwa waliolazwa mpaka sasa, Mathias Kapizo ameitaja hii >>>> “Kwa
takwimu za leo katika wodi ya Makurumla tulikuwa na mgonjwa mmoja…
Ubungo wagonjwa wawili, Mwananyamala wagonjwa watatu, Magomeni mgonjwa
mmoja, Kawe wagonjwa wawili, Manzese wagonjwa watano, Tandale wagonjwa
wawili, Sinza wagonjwa watano, Makongo mgonjwa mmoja, Mburahati wagonjwa
sita, Kigogo wagonjwa wawili, Mbezi mgonjwa mmoja, kutoka Mlandizi
wamekuja wagonjwa wawili, Wazo (Tegeta) mgonjwa mmoja, Makuburi mgonjwa
mmoja, Kimara mgonjwa mmoja, Mabibo mgonjwa mmoja na Tabata mgonjwa
mmoja.” >>>> Mathias Kapizo, Afisa Afya Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam.
Ishu ya mlipuko wa Kipindupindu ilianza
kuchukua headlines tangu asubuhi ya August 18 2015 katika Mitandao
pamoja na Vyombo vya Habari TZ.
0 comments:
Post a Comment