Mitandao ya Kijamii ina nguvu yake kubwa
sana sikuhizi, stori yoyote ikiibuka inasambaa kwa kasi kubwa sana
kupitia mitandao hiyo tena kwa kasi kuliko chombo kingine chochote cha
Habari !!
Rais wa Mexico
alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya picha yake kusambaa ikionesha
amevaa soksi kwa kugeuzia juu chini, yani ile sehemu ya kisigino
inaonekana kama iko kwa juu!
Rais huyo, Enrique Peña Nieto alipigwa
picha katikati ya Mwezi August 2015 wakati akishiriki mbio fupi
katikati ya Jiji la Mexico, camera za paparazzi zikanasa miguuni, alivaa
soksi
nyeupe alafu inaonekana rangi ya kijivu kwa juu… kutokana na
mazoea ya wengi walihisi Mr. President amegeuzia soksi juu chini !!
Baada ya story kuchukua headlines Mitandaoni ilibidi Mheshimiwa aingie kwenye ukurasa wake @Twitter na kuweka picha inayoonesha soksi hizo kuonesha kwamba hakugeuzia, ni muundo wa soksi uko hivyo kwa hiyo watu wasielewe vibaya.
Utani haukosekani, kati ya watu waliocomment baada ya post hiyo aliandika hivi; >>> ‘Asante kwa kutuweka sawa kuhusu hili, sikuweza kupata usingizi kwa sababu ya kufikiria soksi zako’ >>>
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo,
0 comments:
Post a Comment