Stori ninayokusogezea sasa hivi ni hii
kutokea 88.1 Mwanza kuhusu Shopping Mall mpya inayotarajiwa kufunguliwa
wakati wowote ambayo itakuwa ikiitwa jina la rais wa jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwa mujibu wa afisa mahusiano wa jiji la Mwanza
alipokutana na ripota wa millardayo.com..‘Tumeamua
kuita Jakaya Mrisho Kikwete kwasababu ni utamaduni wa muda mrefu kwa
kweli za utamaduni kwamba inapotokea kiongozi akafanya jambo jema na ni
zuri basi vitu uwa vinaitwa kwa jina lake ukaona kuna baadhi ya barabra
zimepewa majina kama ya Kenyatta,Nyerere’ – Joseph Mlinzi‘Katika hili la Jakaya Mrisho Kikwete Shopping Mall ni kwa utambuzi kwamba huyu ni rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambaye ameongoza kwa awamu mbili mfululizo ameweka mchango mkubwa katika nchi yetu kipindi cha utawala wake ikiwa pamoja na utekelezaji mzuri kupitia chama cha Mapinduzi’ – Joseph Mlinzi
‘Shopping Mall hii ni kubwa kwa Afrika Mashabiki na kati kwa mfano ukienda Dar Mlimani city ambayo ina mita za mraba 15000, ukienda Kenya wana Westgate ambayo haifiki mita za mraba 30000, ukienda za Uganda na sehemu zingine, mwisho wa siku tulitaka kufanikisha yale maono ya Mheshimu Rais kwamba katika jiji la mwanza tunaona kitu kizuri bora na kinaelekea kule ambako yeye alisema anataka jiji la mwanza liwe kama California ya Tanzania’ – Joseph Mlinzi
0 comments:
Post a Comment