Kuna stori za baadhi ya Viongozi wa
Africa kung’ang’ania kukaa madarakani hata baada ya vipindi vyao vya
uongozi kuisha, pia wako ambao wanaendelea kuongoza kihalali kutokana na
mabadiliko ambayo wameyafanya kwenye Katiba ili waendelee kuongoza !!
Siku chache zilizopita nilikusogezea
stori kuhusu Rais mwenye umri mdogo kuliko wote Duniani, leo nakupa hii
toka ndani ya Africa… unajua Marais wanaoongoza kwa kuwa na umri mkubwa?
List niko nayo hapa mtu wangu, kila mmoja na picha yake kabisa !!
1. Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ana miaka 91, ndiye Rais mzee kuliko wote, ameshinda urais kwa muhula wa saba
2. Beji Caid Essebsi-Ana miaka 88, amekua Rais wa Tunisia tangu Desemba 31 2014
3. Rais Paul Biya wa Cameroon ana miaka 82, ameingia madarakani tangu mwaka 1982
4. AbdelAziz Boeteflika ni Rais wa Algeria toka April 1999, ana miaka 78
5. Rais wa Guinea Alpha Conde ana miaka 77, amekua madarakani tangu December 2010
6. Rais wa visiwa vya Sao Tome, Manuel Pinto da Costa ana miaka 77, aliingia madarakani tangu mwaka 2011
7. Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ana miaka 76, aliingia madarakani tangu Januari 2006
8. Rais wa Malawi, Peter Mutharika ana miaka 74, aliingia madarakani May 2014
9. Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara ana miaka 73, aliingia madarakani tangu mwaka 2011
10. Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ana miaka 73, aliingia madarakani tangu May 9, 2009
0 comments:
Post a Comment