Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki
(CCM), Bi. Celina Kombani utaagwa rasmi leo Jumatatu, kuanzia majira ya
saa nne asubuhi katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Ofisi ya Bunge, baada ya zoezi la kuaga mwili wa marehemu na kutoa
heshima za mwisho, utasafirishwa kwenda mkoani Morogoro kuanzia majira
ya saa tisa alasiri ambapo utalala nyumbani kwake Forest Hill.
Jumanne kuanzia majira ya saa nne
asubuhi, itafanyika ibada maalum ya mazishi na baadaye mwili utaagwa
katika Viwanja vya Jamhuri mjini Morogoro na kufuatiwa na mazishi
shambani kwake, Lukobe nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Live Updates kutoka Viwanja vya Karimjee, Dar.
Saa 4:45 asubuhi, Mwili wa marehemu Celina Kombani tayari umewasili katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar, kwa kuagwa rasmi.
Saa 5:00 asubuhi, Wasifu wa marehemu Celina Kombani inasomwa.
Saa 5:20 asubuhi, Salam
za pole kwa wafiwa na Watanzania wote zinatolewa na wizara za serikali,
taasisi na mashirika mbalimbali ya umma na serikali.
RSS Feed
Twitter
September 28, 2015
Unknown
0 comments:
Post a Comment