Ligi Kuu Tanzania Bara inaanza Jumamosi hii huku klabu za
Simba, Yanga na Azam zikiwa ndiyo zilizotumia gharama kubwa kwenye
usajili katika msimu huu wa 2015/16.
Dirisha la usajili
wa wachezaji wa Ligi Kuu Bara kwa ajili ya msimu wa 2015/16
lilifunguliwa Agosti 6, 2015 na lilifungwa Agosti 30 mwaka huu.
Wafuatao ni baadhi ya wachezaji waliosajiliwa kwa fedha nyingi kwa ajili ya msimu wa 2015/16 unaoanza mwishoni mwa wiki hii:
Donald Ngoma (Yanga)- Sh105 milioni
Yanga
ilitumia dola 50 (Sh 105 milioni za Kitanzania) kumsajili Mzimbabwe
Donald Ngoma na kumfanya kuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa gharama kubwa
zaidi nchini Tanzania kwa mwaka huu.
Simba
ilitumia Sh 50 milioni kwa ajili ya kumsajili kiungo wake wa zamani,
Mwinyi Kazimoto aliyekuwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake
katika klabu ya Al Markhiya ya nchini Qatar.
Ramadhani Singano (Azam)-Sh50 milioni
Azam
ilitumia Sh 50 milioni kumsajili winga Ramadhani Singano ‘Messi’
aliyekuwa mchezaji huru baada ya kuachana na klabu yake ya zamani ya
Simba. Singano alipewa kitita hicho cha fedha na kumfanya awe mchezaji
mwenye umri mdogo aliyesajiliwa kwa gharama ya juu zaidi msimu huu.
Ame Ally (Azam)-Sh50 milioni
Mshambuliaji
wa Azam, Ame Ally naye amesajiliwa kwa kitita cha Sh 50 milioni
akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, ambapo kiasi hicho cha fedha
kimegawanywa kwa mchezaji na klabu ya Mtibwa kwa makubaliano.
Hamisi Kiiza (Simba)- Sh42 milioni
Hamisi
Kiiza alisajiliwa na Simba kwa gharama ya dola 20,000 (Sh 42 milioni)
akiwa kama mchezaji huru. Awali kabla ya kujiunga na Simba, Kiiza ambaye
ni raia wa Uganda aliwahi kuwa mchezaji wa Yanga kwa misimu minne
mfululizo.
Allan Wanga (Azam)-42 milioni
Mshambuliaji wa Azam, Mkenya Allan Wanga amesajiliwa kwa Dola 20,000 (Sh 42 milioni) akitokea Al Merreikh ya Sudan.
Deus Kaseke (Yanga)-35 milioni
Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania, Yanga ilitumia kiasi cha Sh 35
milioni kumsajili kiungo mchezeshaji Deus Kaseke aliyekuwa akiichezea
Mbeya City.
Malimi Busungu
Mshambuliaji
huyu amesajiliwa na Yanga kwa kitita cha Sh 25 milioni akitokea klabu
ya JKT Mgambo, pia Peter Mwalyanzi naye amesajiliwa na Simba kwa Sh 25
milioni akitokea klabu ya Mbeya City.
0 comments:
Post a Comment