Nimekutana na stori kwenye moja ya mitandao inayoonyesha wanamuziki wa hip hop Marekani Eminem, Kanye West na Jay Z wanafanana kitu kimoja…utumiaji mwingi wa misamiati mikubwa kwenye nyimbo zao.
Eminem
Kutokana na
utafiti mpya uliofanyika, wasanii hawa wa tatu ni miongoni mwa wasanii
tano bora wenye misamiati mingi zaidi kwenye industry ya muziki Marekani. >>>“Nia ni kulinganisha ukubwa wa utumiaji wa misamiati wa hawa wananuziki”<<< hii ni nukuu ya moja ya sentensi kutoka kwenye utafiti huo .
Jay Z
Kuna baadhi
yao wamefanikiwa kuwa na idadi kubwa ya mashabiki mpaka leo kwasababu ya
sanaa yao na jinsi ambavyo wameweza kutumia misamiati kuwagusa
mashabiki…Utafiti huo umetumia orodha ya wasanii 99 bora duniani,
wamelinganishwa na kuchujwa kwa kuhesabu idadi ya misamiati ya kipekee
waliotumia kwenye nyimbo zao zote.
Eminem aliibuka kidedea akiwa na idadi ya misamiati 8,818 ya kipekee kwenye nyimbo zake akifuatiwa na rappa Jay Z akiwa na idadi ya misamiati 6, 899 , Marehemu Tupac Shakur akiwa na idadi ya misamiati 6,569 na Kanye West akiwa na idadi ya misamiati 5,069.
Mtunzi wa nyimo Bob Dylan ameshika nafasi ya tano akiwa na idadi ya misamiati 4,883 na ni msanii pekee asiyefanya muziki wa hip hop kushika nafasi hiyo. Kitendo cha wasanii wa Hip Hop
kushika nafasi zote 4 za juu pengine sio kitu cha kushangaza sana kwani
wengi tunafahamu kuwa asili ya muziki wa Hip Hop umejengwa kwenye
misingi ya kutumia mistari yenye misamiati migumu.
Wewe unauonaje uchambuzi huu mtu wangu? unakubaliana na hii orodha ama unahisi ni msanii gani wa Hip Hop Marekani anatakiwa pia kuwepo kwenye hii 5 bora?
RSS Feed
Twitter
August 07, 2015
Unknown
0 comments:
Post a Comment