Monday, August 3



Elizabeth Michael 'Lulu'.
Makala: Deogratius Mongela
Umaarufu na ustaa wao kamwe haulingani na matunda ya kazi zao! Unajua kinachowabeba na kuwaweka mjini baadhi ya mastaa Bongo? Ni muonekano wa shepu na maumbo bomba waliyojaaliwa na Mwenyezi Mungu!

KHADJA SAID ‘KADIJANITO’
KHADJA SAID ‘KADIJANITO’
Mwanadafada Khadja Said ‘Kadijanito’ kutoka Nyumba ya Vipaji (THT) alitusua na ngoma ya Maumivu na kumtambulisha vema katika ramani ya muziki wa Bongo Fleva kwa kuliteka gemu na kujihakikishia nafasi ya kupendwa na mashabiki wa muziki huo kutokana na uwezo wake, ingawa anatajwa kama msichana mwenye mvuto kwa wanaume.

ESTER KIAMA
Ni staa wa kike kutoka kiwanda cha filamu Bongo. Ester ameweza kupenya kwa kasi na kuwapa presha mastaa wakongwe wa kike wa tasnia hiyo kutokana na ulimbwende wake kwa kuwadatisha vikali wanaume kutokana na staili yake ya kupenda kuvaa nguo fupi. Ester anadaiwa kutoka kimalavidavi na msanii nguli na mtayarishaji wa filamu, Kulwa Kikumba ‘Dude’.


ASHA SALUM ‘KIDOA’
Kidoa ni video queen aliyepenya kupitia Ngoma ya Akadumba ya staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na kuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kutokana na muonekana wake ulioleta ushindani kwa mastaa wengine huku baadhi wakidai kuwa umbo lake siyo la asili bali la dawa za Kichina.

LULU SEMAGONGO ‘AUNTY LULU’
Aunty Lulu alishawahi kuwa Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha C2C, baadaye akaibukia kwenye filamu za Kibongo na kupenya kiulaini huku umbo lake likitajwa kumbeba zaidi. Pia alishawahi kuandikwa kutoka kimapenzi na mwigizaji mwenzake, Bond Bin Suleiman ambaye ni meneja wa msanii Wastara Juma.

AGNESS GERALD ‘MASOGANGE’
Masogange anatajwa kuwa miongoni mwa wanawake wenye mvuto wa kimapenzi na kivutio kikubwa cha wanaume kutokana na umbo lake. Mwanadada huyo alipata umaarufu na kubaki kileleni baada ya ‘kushaini’ kwenye ngoma ya Masogange ya msanii Abednego Damian ‘Belle 9’, mwaka 2008 na kuteka anga la Bongo Fleva. Alishawahi kukwaa skendo ya kutoka na msanii Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ wa Kundi la Tip Top Connection.

ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’
Staa ambaye nyota yake ilianza kung’ara tangu utotoni kupitia michezo ya runingani na kuendelea kukua kwa kasi kubwa na kuweza kutingisha tasnia ya filamu Bongo.
Lulu anatajwa kuwa ndiye mrembo pekee ambaye alishawahi kuingia katika kinyang’anyiro cha warembo wenye mvuto Afrika Mashariki huku akikwaa skendo mbalimbali ikiwemo ya kutoka na marehemu Steven Kanumba.

0 comments:

-