Bi harusi Agnes Omari akiombewa baada ya kupandisha mashetani.
Chande Abdallah na Deogratius Mongela
Mshtuko! Bi harusi Agnes Omari (26) amezua kizaazaa baada ya kudaiwa
kupandisha mashetani kanisani wakati akivishwa pete ya ndoa, hali
iliyosababisha tendo la kufungishwa ndoa kusimama kwa muda kwa ajili ya
kutafuta msaada wa maombi.
Akizungumza
na Ijumaa Wikienda, bwana harusi, Arnold Martin alisema sakata hilo
lilijiri hivi karibuni kwenye Kanisa Katoliki la Parokia ya
Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Alisema
kwamba, alipata taarifa usiku wa kuamkia siku ya ndoa kutoka kwa
msimamizi wa bi harusi kuwa mchumba’ke amepandisha mashetani, tatizo
ambalo hakuwa nalo katika kipindi chote walichoishi pamoja.
Kutokana na tatizo hilo, Arnold alisema alivunja utaratibu na kwenda
kumuona mchumba’ke huyo na kumkuta akijigaragaza huku akipiga makelele
na kuzungumza lugha za ajabu.
“Kulipokucha,
hali yake ilionekana kuwa nzuri kiasi kwamba majira ya saa 3:00
asubuhi, aliondoka na msimamizi wake kwa ajili ya kubadilisha gauni la
harusi maeneo ya Mbagala-Kizuiani baada ya lile la awali kuonekana
kumbana huku na mimi nikijiandaa kwenda saluni,” alisema Arnold.
Baada ya kutoka na msimamizi wake huyo,
haukupita muda mrefu akapigiwa simu kuwa hali hiyo imejirudia, akamfuata
na kumbeba kwenye gari lake kisha kumkimbiza katika Parokia ya
Mbagala-Zakhem kwa ajili ya msaada wa maombi na kutoa taarifa kwa paroko
kuhusu hali ya mchumba’ke huyo.
Bi
harusi huyo aliombewa lakini wakati akimvisha pete ya ndoa kanisani
hapo hali hiyo ilijirudia ndipo alipohamishiwa katika Kanisa la Nabii
Yaspi lililopo Buza-Kipera jijini Dar ambapo wakiwa huko, walikutana na
wachungaji ambao waliwaombea na hali ikatulia.
“Hali
hiyo ilijirudia tena wakati tukipiga picha palepale kanisani akaanza
tena kupandisha mashetani, akaombewa lakini hali ilizidi kuwa mbaya,
wakaja watu wa Karismatiki nao ikashindikana ikabidi tufunge safari tena
kuelekea kulekule kwa Nabii Yaspi ambako aliombewa, akapona.
“Wakati tukiingia ukumbini, hali hiyo
ilijirudia tena ambapo sherehe nzima iliharibika na kuwa majonzi hivyo
kila mtu akaondoka kimyakimya.
“Bi
harusi aliondoka na ndugu zake usiku ule hadi kesho yake nilipoambiwa
amerudia hali yake ya kawaida ila kinachonishangaza nilipoenda pale
nyumbani kwao alikuwa akionesha kama vile hanifahamu kabisa pamoja na
kwamba nilifunga naye ndoa,” alisema Arnold ambaye alidai kuwa
anatarajia kurudi tena kwa Nabii Yaspi ili kumaliza tatizo hilo.
0 comments:
Post a Comment