Monday, July 6



Baada ya kuachia kisebusebu na noma ,Band ya muziki wa kizazi kipya inayotamba nchini Ruby Band inajipanga kuachia video ya wimbo mpya kabla ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani na pia wanatarajia kuachia wimbo wao mpya waliomshirikisha  msanii mkubwa hapa nchini ambaye wamemtambulisha kawa  ‘’KING’.
Jina hilo KING bado uongozi wa ruby band haujaweka wazi ni king yupi.lakini wengi wamekuwa wakisema huenda vijana hao wamefanya colabo la hatari na ALIKIBA ambaye kwa sasa ndiye anayejiita KINGKIBA.

Hata hivyo mmliki wa band hiyo ruby yusuph maarufu kama Madam Ruby hajataka kuweka wazi juu ya KING yupi kashirikishwa na vijana hawa.
‘’naomba mashabiki wa ruby band wakae mkao wa kula tu,kazi nzuri ya vijana inakuja na watu wajue tu ni ruby band featuring KING.Mengine watajua wimbo ukishatoka,tunatarajia utatoka baada ya ramadhani ila video ya wimbo mwingine tutaiachia hivi karibuni muda wowote kutoka sasa...alisema madam ruby.
RUBY BAND ni band inayoundwa na vijana wanne ambao tangu waingie katika soko la muziki wa Tanzania wamekuwa wakitoa changamoto kwa wasanii wa muziki wa band wakiwa ni moja ya band chache zinazofanya vizuri katikamuziki wa bongo flavour.
Wimbo wao wa kwanza unaitwa kisebusebu na wa pili unaitwa noma ambazo zote zina video.pia wamekuwa wakitunga nyimbombalimbali zinazohamasisha masuala ya kijamii kama ‘kitu kimojaúliokuwa unahimiza kupiga vita mauaji ya albino.


0 comments:

-