Monday, July 6


 Hii ndio filamu ya Wake Up iliyomaliza bifu la wasanii Hemed na Mlela ebu bonyeza uione live bila king'amuzi
  Wasanii Hemed na Yusuph Mlela walipokutana uso kwa uso wakati wakiigiza filamu ya Wake Up iliyosheheni mastaa zaidi 30
  Msanii Yusuph Mlela



 Msanii Manaiki Sanga
Lile bifu lililokuwa limeshika kasi kubwa kati ya wasanii wenye majina hapa mjini Yusuph Mlela na Hemd Suleiman hatimae bifu hilo limekweisha kabisa baada ya wasanii hao kuamua kuweka silaha chini na kuungana kutengeneza filamu moja iitwayo Wake Up ya msanii mwenzao Maniki Sanga ambayo inatarajia kuachiwa mwanzoni mwa mwezi ujao huku Kampuni ya Steps ikisimamia kuisambaza.














Na Mwandishi Wetu
Msanii mwenye jina kubwa nchini kwenye kiwanda cha Bongo Movie Vicent Kigosi maarufu kwa jina la Ray ameibuka na kumpongeza msanii  mwenzake Manaiki Sanga kwa kuandaa  filamu bora  na ya kwanza katika histori ya filamu kwa kuchezwa na mastaa zaidi ya 30 kwa mpigo.
Akiongea na mtandao huu Ray alisema “ Kaka huwa ni vigumu kwa baadhi ya wasanii kusifia kazi ya msanii mwenzao  lakini mimi nazungumza toka  moyoni kuwa filamu ya Wake Up ni filamu ya kwanza kuwa na uboro huku ikiwa imesheni mastaa wengi kupita kiasi” Alisema Ray
Aidha msanii huyo aliongeza kusema kuwa Manaiki Sanga anastahi pongezi kwa kazi nzuri na wasanii wote wanatakiwa kumuunga mkono kwani licha ya uchanga wake kwenye tsania hiyo lakini ameweza  kuleta upinzani mkubwa kwa wao mastaa kiasi cha kuwafanya kuumiza kichwa muda wote.

Filamu ya Wake Up ambayo itasambazwa na kampuni ya Steps na inatarajia kuwa mtaani mapema mwezi ujao huku maelfu ya mashabiki wakiisubiri  kwa hamu kuona  ushiriki wa mastaa wengi. 

HII NDIYO FILAMU MPYA YA "WAKE UP" YA MSANII MANAIKI SANGA AMBAYO MASTAA ZAIDI YA 30 WAMESHIRIKI HUMO..!


UWOYA NA MANAIKI NDANI YA FILAMU HIYO MPYA INAYOTA

0 comments:

-