Monday, July 6




Rapa wa kike anayekuja kwa kasi katika industry ya muziki wa Tanzania chemical a.k.a myself anayetamba na wimbo wake sielewi ft soprano ameweka wazi kuwa yupo katika mahusiano ya kimapenzi na boyfriend wake na siyo kama watu wengi wanavyomfikiria kutokana na  muonekano na uvaaji wake wa kiume.

Msanii huyo amesema taarifa za mitazamo mibaya iliyopo kwa baadhi ya watu kutokana na muonekano wake na uvaaji wake wa nguo za kiume si za kweli na  kwamba yeye ana boyfriend na anampenda ila uvaaji wake unatokana na hassle zake tu na wakati mwingine analazimika hadi kutembeakwa miguu katika mihangaiko yake.
Kuhusu kazi zake na kujiingiza kufanya hiphop amesema  anavutiwa na kutamani sana kufanya kazi na msanii nguli wa hip hop hapa bongo  farid kubanda a.k.a fid q.


Chemical ambaye kupitia wimbo wake wa sielewi ameweza kupata air time ya kutosha katika vituo mbalimbali vya televisheni hapa nchini akiongea na kituo cha mlimani tv amesema fid q ni rapa aliyemshawishi kuingia katika game ya muziki na tangu akiwa mdogo amekuwa akiimba na kuchana ngoma za msanii huyo ikiwemo fid q.com na nyinginezo.


Amesema pia kuwa mafanikio yake yanatokana na management yake pamoja na saport ya kutosha anayoipata kutoka kwa wazazi na ndugu zake bila kusahau mashabiki amabo wamempokea kwa mikono miwili kama mmoja wa marapa wa kike.

Chemical anakuwa moja ya wasanii wa kike wachache wanao rap akifuata nyendo za marapa wengine kama chiku keto,rah p na wengine ambao hata hivyo harakati zao siyo kubwa sana ukilinganisha na marapa wa kiuume.

Hata hivyo ameahidi mashabiki wake kuendelea kukaza zaidi na kamwe hawezi kuacha muziki.



0 comments:

-