Sunday, July 19



Ile  couple  ya  wasanii  wa  kibongo  wasioishiwa  skendo, Shilole  na  Nuh  Mziwanda  imeubuka  upya  kwa  staili  ya  kipekee.
Tumezoea  kusikia  Shilole  kamnasa  makofi  Mziwanda, mara  kampiga  chupa  na  mengine  mengi ya  aina  hiyo.
Awamu  hii  wamekuja  na  mpya  ya  kuchambana  live  mitandaoni. Nuh  kafananishwa  na  ganda  la  ndizi  huku  Shilole akifananishwa  na  Asha  Ngedele......

Aliyelianzisha  Varangati  hili  ni  Shilole, ambaye  ameandika  ujumbe  huu  instagram.
 
"Mwanaume hata umfanyie nini haridhik lol! Pamoja na kukubali shida zake zote lakin mh! Nimejitahid nimehangaika'ila sasa kama gari limewaka'aka babu weeee kanikuta na maisha yangu wacha niendelee na maisha yangu'Mimi na yeye baaaaaaasi #GaNdALaNdiZi .™@shilolekiuno"

Nuhu nae akaona isiwe tabu akamwaga ugali, na kachumbari

"Mwanaume wa kweli ukaa kimya'sibishani na upumbavu'mwanamke asieridhika na kujua kua kathaminiwa mpaka tatoo kachorwa'na kuvumilia mambo yote alionifanyia ya kuniaibisha mbele ya mashabiki zangu'familia na'wasanii wenzangu na wadau'anaanza kunitukana mitandaoni for whaaaat!!! Mxeeeeew'mimi bado kijana na nna time ya kupata maisha yangu na mtu atakae thamini moyo wangu 'nawaachia wanaume wenzangu na nyie mjaribu zari 'mimi nacheka tu #AsHaNgeDerE. ™@mziwandanation"
 


0 comments:

-