Kenya imetajwa kwenye Top Ten ya nchi
Tajiri Afrika 2015, hiyo ni good news.. Zimebaki wiki kama tatu hivi ili
tushuhudie Rais wa Marekani, Barrack Obama anatembelea nchi hiyo, hiyo ni good news.. lakini ziko story upande wa pili wa shilingi pia.
Kama wewe ni mtazamaji wa Taarifa za
Habari kwenye TV za Kenya itakuwa umeshuhudia pia majanga ya pombe za
kienyeji, wapo wanaofariki, wengine wanajikuta hali mbaya mpaka
wanalazwa Hospitali, lakini bado kuna wengine wanaendelea
kutumia vilevile!!
Moja ya vitu vilivyonishtua ni hii
kukutana na chupa ya Pombe ambayo wanasema hata haijasajiliwa na inauzwa
kama kawaida. jina lake je? >> Inaitwa ‘Rest in Peace Premium Vodka‘ na kuna picha ya Jeneza kabisa kwa chini yake.
Serikali ya Kenya haijaliacha hili
lipite, Vikosi vya Wanausalama wako kazini kuhakikisha wanafanikiwa
kabisa kumaliza tatizo la Viwanda vya Mitaani vinavyozalisha pombe za
Kienyeji.
Hapa iko na list ya Viwanda na aina ya Pombe ambazo Serikali ya Kenya imezipiga MARUFUKU !!
0 comments:
Post a Comment