Upigaji wa picha za selfie Umeendelea kupata umaarufu kila siku duniani kutokana na kazi ya teknolojia inayozidi kukua.
Kila mtu anatamani kuwa na simu ya Smartphone ili tu aweze kupata urahisi wa mawasiliano pamoja na upigaji wa picha hizo.
Hii imetokea kule Romania baada ya binti wa miaka 18 Anna Ursu
na wenzake kujaribu kupiga picha juu ya treni inayotembea ili wapate
picha ya selfie ya kipekee lakini kilichotokea ni kingine baada ya
kupigwa na shoti ya umeme wakiwa juu ya treni hiyo.
Wasichana wawili walibahatika kuokolewa na kukimbizwa hospitali lakini mwili wa Anna Ursu ulikua umeuungua kwa kiasi kikubwa huku wenzake wakiwa na majeruhi machache na baada ya muda kidogo alifariki.
Madaktari wamesema kwamba Anna
alipigwa na shoti ya umeme na nyaya zilizokua zimepita juu wakati wa
tukio hilo la picha na kusababisha volt 27,000 kutembea kwenye mwili
wake na kusababisha mwili wake kua kama transfoma ya umeme hivyo kua ngumu kupona kwa kuwa alikua na uwezo wa kumlipua mtu yoyote atakaye mgusa.
0 comments:
Post a Comment