May 24 mwaka huu itakua ni Anniversary ya mastaa Kim Kardashian na Kanye West baada
ya kutimiza mwaka mmoja wa ndoa yao ambayo walifunga mwaka jana katika
sherehe iliyofanyika Italy na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Wawili hao ambao kwa sasa wana mtoto mmoja aitwaye North West wamepanga kuhitimisha siku hiyo kwa kurudia viapo vya ndoa yao katika mnara wa Eiffel uliopo jijini Paris, Ufaransa.
Kanye ambaye
kwa sasa anajulikana kwa jina la Dk. Kanye West amepanga kufanya kitu
cha tofauti katika siku yao hiyo muhimu ambayo itahudhuriwa na watu wa
karibu zaidi ambao ni wanafamilia.
0 comments:
Post a Comment