WAZIRI wa kilimo, Chakula na Ushirika Steven Wasira amewafukuza kazi wakurugenzi watendaji watatu wa Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (Yaani Rufiji River Basin Development Authority – RUBADA) kutokana na matumizi mabaya ya ofisi ya Umma ambayo yameitia hasara ya Bilioni 2.5 Serikali .
Akitoa
agizo hilo leo mbele ya Waandishi wa Habari, Waziri Wasira amewataja
Watendaji hao kuwa ni Bwana Aloyce L. Masanja – Kaimu Mkurugenzi Mkuu;
Bibi Tabu Ndatulu – Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji; na Bwana Filozi
John Mayayi – Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.
Wassira
amesema baada ya Ofisi yake kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wa
vijiji vya Rufiji pamoja na wawekezaji juu ya Urasimu wa shirika hilo,
aliunda timu ya Uchunguzi kutoka wizara ya Kilimo na Hazina kwenda
kuchunguza malalamiko hayo.
“Baada
ya kuunda tume kutoka hapa Wizarani ikishirkiana na Hazina,
walienda kwenye shirika hilo kufanya ukaguzi.Tume ilibaini kwamba
mfumo wa pale ulikuwa ni mbovu, wakurugenzi hawa walijifanya
wahasibu, wakawa wanakuanya pesa wenyewe na kutembea
nazo.Walifanya maksudi tu ili kujiwekea mianya ya kuiba Fedha” Amesema Wassira
Taarifa
ya Mheshimiwa Wasira imeanisha kuwa kati ya shilingi 2.748 billion
zilizokuwa zimekusanywa kwa ajili uwekezaji, ni shlingi 714.606 milioni
tu ndizo zimetumika kihalali wakati kiasi kilichobaki kimetumika bila
kuzingatia sheria na kanununi za fedha za umma.
Waziri
Wassira amesema kuwa mbali ya kuiba pesa hizo, kamati ilibaini kwamba
watendaji hao wametumia zaidi ya Milioni 314 kwenye matumizi yaliyo
kinyume cha utaratibu
ikiwemo pesa zilizotengwa kwa ajili maendelea ya miradi ya Shirika hilo ambazo zimetumika ndivyo sivyo.
Vilevile
Waziri Wassira amesema hata pesa ambazo wamewakata wafanyakazi kwa
ajili ya kupelekwa kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii zimekuwa zikiliwa
na watendaji , tena kwa makusudi pasipo kupelekwa huko.
Aidha,Waziri
Wasira amesema baada ya kupata Ripoti ya Tume hiyo ameiagiza Bodi ya
shirika la Ludaba kuwafukuza kazi mara moja watendaji hao watatu na
nafasi zako kujazwa mara moja huku taratibu na sheria za kuwafikisha
mahakamani zikifanyika.
0 comments:
Post a Comment