Picha Ya Maktaba |
Mkazi mmoja wa Kijiji cha Ulowa Kahama, Chausiku Hamis ameuawa kwa kuchomwa moto na watu waliokusanyika katika msiba wa mtoto wa jirani baada ya kutuhumiwa kuhusika na kifo cha mtoto huyo.
Mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja
alifariki usiku katika mazingira tata ambapo mwanamke huyo aliuawa baada
ya mmoja wa waombolezaji kupandisha mapepo na kumtuhumu Chausiku kuhusika na kifo cha mtoto huyo.
Diwani wa Kata hiyo amesema alipata
taarifa za mtoto huyo kuuawa na baadaye kuuawa mwanamke aliyetuhumiwa
kuhusika na tukio hilo ambapo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Mtendaji
wa Kitongoji hicho walikamatwa na Polisi baada ya nyumba za watu wote
kukimbiwa baada ya tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Shinyanga, Justus Kamugisha amethibitisha tukio hilo kutokea na kusema kuna watu wawili waliokamatwa kwa ajili ya upelelezi.
0 comments:
Post a Comment