Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha nne uliofanyika Novemba mwaka jana, umekamilika.
Katibu mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde
aliliambia gazeti hili wiki hii kuwa “usahihishaji umekamilika na baraza
lipo katika uchambuzi wa kuyapanga na tutakapokamilisha tutayatangaza”.
Alipoulizwa ni lini hasa matokeo hayo
yatatangazwa, Dk Msonde alisema: “Tumemaliza kusahihisha na mchakato wa kuyapanga ukikamilika tutawaeleza hivyo msiwe na shaka.”
yatatangazwa, Dk Msonde alisema: “Tumemaliza kusahihisha na mchakato wa kuyapanga ukikamilika tutawaeleza hivyo msiwe na shaka.”
Katika kipindi cha miaka miwili mfululizo, mwaka
2012 na 2013, Necta ilitangaza matokeo ya kidato cha nne mwishoni mwa
Februari na mwanzoni mwa Machi.
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika
mwaka 2013 yalitangazwa Februari 22, mwaka jana na 2012 yalizua gumzo
kutokana na asilimia 60 ya watahiniwa kufeli.
Kwa kawaida, muhula wa masomo kwa kidato cha tano
huanza Julai, huku Machi na Aprili mchakato wa kuwapangia shule
hufanyika wakati Mei na Juni hutumiwa kwa maandalizi kwa wanafunzi hao.
Katika matokeo ya 2013 kama ilivyokuwa katika
matokeo ya mwaka 2012, shule binafsi zilikuwa na matokeo mazuri
kulinganisha na za Serikali zilizokuwa zikitamba miaka ya nyuma.
Kwa mujibu wa Necta, matokeo ya mwaka 2013, shule
kongwe za Serikali na zile za vipaji maalumu, zilishindwa kuingia kwenye
orodha ya shule 30 bora.
Shule kongwe kihistoria zimekuwa zikitoka kapa
katika matokeo ya Mtihani wa Taifa. Tofauti na matarajio ya wengi, shule
hizo nyingi hazikuwamo hata katika orodha ya shule 100 bora.
Baadhi ya shule hizo ni Fidel Castro ambayo
ilishika nafasi ya 83, Malangali (172), Ifunda Ufundi (205), Jangwani
(226), Bwiru (242), Songea Wavulana (257), Pugu (325) na Azania (333).
Ikiwa ni mwaka mmoja umekamilika tangu Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ulipoanzishwa, taasisi ya Hakielimu ilitoa
matokeo ya utafiti wake yanayoonyesha hakuna kilichofanyika.
Kaimu Mkurugenzi wa HakiElimu, Godfrey Boniventura
alisema Serikali isitumie kigezo cha kuongezeka ufaulu kama ishara
tosha ya kuimarika kwa elimu, kwani licha ya ufaulu huu kuonyesha
kupanda ghafla, kuna changamoto nyingi katika sekta hiyo ambazo bado
hazijatatuliwa na juhudi kubwa zinahitajika.
“Mfano migogoro ya mara kwa mara kati ya walimu na mwajiri, utoro wa walimu, ukosefu wa maabara, vifaa vya kufundishia na tofauti kubwa iliyopo katika gharama za utoaji elimu nchini kati ya shule za serikali na shule za binafsi,” alisema Boniventura.
“Mfano migogoro ya mara kwa mara kati ya walimu na mwajiri, utoro wa walimu, ukosefu wa maabara, vifaa vya kufundishia na tofauti kubwa iliyopo katika gharama za utoaji elimu nchini kati ya shule za serikali na shule za binafsi,” alisema Boniventura.
0 comments:
Post a Comment