Tuesday, February 3

NI shida! Wakazi wa Mlandizi mkoani Pwani mwishoni mwa wiki iliyopita walijikuta wakishinda nje ya nyumba moja ya kulala wageni iitwayo Kilimahewa Guest House baada ya kuwepo taarifa za watu wawili, mtu na mpenzi wake kunatana baada ya kudaiwa kufanya mapenzi majira ya asubuhi.

Mwananchi akitumia tochi kuwasaka uvunguni.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, taarifa za kuwepo kwa tukio hilo zilisambaa kwa kasi na chanzo chake kinadaiwa ni mwendesha pikipiki mmoja aliyetoa habari hizo.

Kutokana na uvumi huo, mamia ya watu walijazana nje ya nyumba hiyo,  huku wakisisitiza kutaka kuwaona watu hao.“Saa 3 asubuhi kuna mtu mmoja wa pikipiki alikuja akatuambia kuwa watu wamenasiana katika Gesti ya Kilimahewa, huwezi amini watu wametoka Chalinze kwa ajili ya tukio hili na sisi  harakaharaka tukafika hapa kuona nini kinaendelea, mpaka sasa hatujui kama ni kweli ama sio kweli.
“Polisi wamefika hapa wamesema hakuna ukweli baada ya kuikagua gesti nzima lakini hata hatuamini tupotupo tu,” walisema baadhi ya akina mama waliokuwa nje ya gesti hiyo, waliodai wametokea Chalinze.
Diwani wa Kata ya Janga (CCM), Mlandizi, Fedilia Swai alifika eneo la tukio baada ya kupokea taarifa  na kukagua kila chumba na aliwaambia wananchi kuwa hakuona chochote ndani ya gesti hiyo na kwamba huo ni uvumi ambao hauna ukweli wowote na kuwataka watu warudi makwao.

Muonekano wa kitanda walichokuwa wakitumia wapenzi hao.
“Unajua muda huu nilikuwa katika shughuli nyingine, lakini ilinibidi nifike hapa baada ya kupata taarifa kuwa kuna wananchi wangu wamenasiana. Nimeingia vyumba vyote hakuna kitu kama hicho nimeingia na mashahidi wawili, mwanaume mmoja na mwanamke mmoja tumekagua kote hakuna watu hao.
 Nasisitika hizi taarifa ni za uongo tena uzushi mkubwa.”

Kauli ya diwani huyo haikutosha mpaka pale alipokuja tena mwenyekiti wa eneo hilo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Kilindo Ahmed ambaye pia alitoa kauli kama hiyo na kuwataka wananchi hao kuteua wawakilishi wawili kwa ajili ya kwenda kuthibitisha ndani ya nyumba hiyo.
Pamoja na mashahidi hao kueleza ukweli wa kutokuwepo kwa tukio hilo, bado wananchi hawakuamini.
Kwa upande wake, mmiliki wa nyumba hiyo, Abdallah Saidi alikanusha taarifa hizo na kusema kuwa amefanyiwa hujuma ili akose wateja katika biashara yake.


...Wananchi wakisubiria kwa nje.
“Kuna watu wamesambaza uvumi huu makusudi ili kuniharibia biashara yangu, huu ni mpango wa kunichafua kibiashara, angalia siku nzima sijafanya kazi yoyote, wateja wangu wataanza kuogopa kuja,” alilalama mmiliki huyo.

0 comments:

-