Thursday, January 22

madonna (1)
Moja ya story iliyosikika masikioni mwa wengi wiki iliyopita ilikuwa ishu ya namba za simu za mastaa AY na Fid Q kuwa hacked, leo kuna hii nyingine ya staa wa muziki kutoka Marekani.

Madonna naye kakumbwa na tatizo hili, system ya computer yake imekuwa hacked na mtu kisha akavujisha albu
m ya 13 ya msanii huyo ya ‘Rebel Heart’ na kuuza nyimbo hizo mtandaoni kwa wizi.

Polisi wa Israel wamemkamata jamaa anayetuhumiwa kufanya hacking hiyo, wanasema ameshafanya wizi wa aina hiyo kwa mastaa wengi wakubwa duniani ambao hawajatajwa majina.

Madonna kawashukuru wote waliosaidia kukamatwa kwa jamaa huyo huku akisema kuwa wizi huo umemvunja sana moyo.

0 comments:

-