#Selfie neno la Kimataifa kwa Mwaka 2013, hiyo ilikuwa majibu ya kazi ya Oxford Dictionaries.
Tangu kumekuwa na mtandao wa Instagram, nimegundua kwamba mtandao huo umekuwa na nguvu zaidi kuipita mitandao mingine ya kijamii ambayo ilitangulia kuwepo kama Facebook na Twitter, tunayaona mengi Instagram, ndiko ambako tuliona pia ile ishu ya kuvuja kwa Selfie ya Malia Obama akiwa amevaa Tshirt ya Kundi la washkaji wanaofanya Hiphop Marekani, Pro Era.
Bado hali si shwari, washkaji wa Kundi hilo walipost picha ya Malia
akiwa amevaa Tshirt hiyo kwenye ukurasa wao Instagram, halafu
wakaandika ujumbe wa kufanya promo ili watu wakanunue Tshirt zao;
“Malia Obama rocking that classic Pro Era tee! | Make sure you get your official Pro Era gear from theproera.com!“– @proera47
“Malia Obama rocking that classic Pro Era tee! | Make sure you get your official Pro Era gear from theproera.com!“– @proera47
Michelle Obama aliwahi kusema anajitahidi kuwadhibiti watoto wake kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii, aliwaruhusu kutumia Facebook tu, hii imevuja na imeenda mbali zaidi ni kwamba Pro Era
wametumia picha hiyo kutangaza bidhaa zao huku wakisema picha hiyo
walipewa na jamaa ambaye ni mmoja wa wanaounda kundi hilo ambaye ni
rafiki wa Malia.
Hali si shwari bado, Maafisa Usalama ndani ya White House wanachunguza
chanzo cha picha hiyo kuvuja, tatizo jingine linaweza kuwa kwa Pro Era, kwanini waitumie picha hiyo kibiashara!
0 comments:
Post a Comment