Hamisa Hassan Mobeto ambaye ni model na actress anayesusua katika tasnia ya filamu nchini anadaiwa kuwa mapenzini na Diamond Platinumz a.k.a Sukari ya warembo huku uhusiano wao ukidaiwa kuwa wa muda mrefu tu ila wamefanya kuwa siri.
Chanzo kimoja kilichodai kuwa karibu na Hamisa ambaye alishawahi kushiriki Miss Tanzania kiliuambia mtandao huu "Hivi mnajua kuwa Diamond anawachanganya kwa wakati mmoja Wema na Hamisa Mobeto?, Hamisa na Diamond ni wapenzi muda sasa but wanafanya siri, Hamisa anamwangalia tu Wema akiwewesekea penzi la Diamond huku yeye akijilia vyake"
Hamisa alipotafutwa na mtandao huu ili kutolea ufafanuzi madai hayo hakuweza kupatikana lakini habari za uhakika ambazo Swahiliworldplanet imezipata ni kuwa kwasasa Hamisa yupo nchini Nigeria lakini haijajulikana kama yupo nchini humo kwa issue gani
0 comments:
Post a Comment