Kimya
cha miezi sita huenda kikarudi na mengi kumhusu mkali Robyn Rihanna
Fenty a.k.a Rihanna, ambaye imeripotiwa kuwa amerudi tena katika mtandao
wa Instagram kuungana na fans wake zaidi ya milioni 12 baada ya
kuwatelekeza kwa kipindi cha miezi 6 ambapo picha ya mwisho kuiweka
katika akaunti yake ilikuwa Mei 3 mwaka huu.
Tangu arudi saa 24 zilizopita tayari ame post picha 11 kwenye ukurasa wake.
Rafiki wa karibu wa Rihanna mwanamitindo
Tom Ford amesema kujitoa kwa msanii huyo Instagram ilikuwa hasara kubwa
kwa kupoteza wapenzi biashara yake ya fashion, hivyo kurudi kwake
kutasaidia kuiokoa hasara hiyo kwa kiasi kikubwa.
Instagram wamemkaribisha Rihanna kwa
mikono miwili kupitia ukurasa wao wa Twitter kwa kuandika, “Welcome back
@rihanna! #RIHunited #badgalback”– Instagram
0 comments:
Post a Comment