DUNIA
hii basi tena! Ni tukio la kusisimua ukilisoma mwanzo hadi mwisho
lakini ni la kikatili sana! Ni lile la ndugu wawili warembo, dada na
mdogo wake kukutwa wamekufa kwa kunyongwa ndani ya nyumba aliyokuwa
amepanga mmoja wao huku muuaji akidaiwa alivaa taulo lenye weupe wa
kufifia akitokomea zake.
Tukio
hilo la kusikitisha lilitokea hivi karibuni kwenye Mtaa wa Mji Mpya,
Kata ya Azimio wilayani Temeke jijini Dar es Salaam ambapo warembo hao,
Mariam Buruhani (39) na dada yake Nuru Tumwaga (42) (pichani) walikutwa
wamekufa katika nyumba hiyo aliyopanga Mariam.Uwazi kama lilivyo kawaida yake, baada ya kuipata taarifa za kuwepo kwa vifo hivyo vya usiku mmoja, lilianza kufuatilia hatua kwa hatua.Kwa mujibu wa ndugu mmoja, mchana wa kuelekea siku ya tukio ambayo ni Jumamosi usiku, marehemu wote walionekana wakiwa wazima wa afya ambapo Mariam alikuwa kwenye saluni yake ya kike na Nuru akiendelea na shughuli zake za kuwaremba wanawake wenzake.
Ikadaiwa kuwa, nje ya saluni ya Mariam kulikuwa na gari dogo jeusi ambalo huwa linapaki maeneo hayo kila wakati ikisemekana mmiliki wake ni bwana wa Mariam ambaye jina halikufahamika mara moja.SOMA ZAIDI>>>
0 comments:
Post a Comment